Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kuhusu kubomolewa choo chake na kuwekwa kwa uzio wa seng’enge na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo
Baadhi ya Wananchi wa Kitogoji cha  Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakipita  pembezoni mwa uzio wa senyeng’e iliowekwa na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo.
Mkazi wa Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Ally Kidunda, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliokuwa uzikutanishe pande mbili za wakulima wa kijiji hicho na mzungu anayemiliki kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayodai kununua shamba katika kityongoji cha Kinyenze na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia ya kwenda mtaa wa Mwanga. (Picha na Mroki Mroki). Kwa habari zaidi Bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duh! Hata njia pia kauziwa. "No Trespassers" inaingia taratibu!

    ReplyDelete
  2. Hili suala la ardhi litaifikisha nchi hii mahali pabaya. Serikali imeridhika na kejeli zinazotolewa na raia wa kigeni kwamba tuna ardhi kubwa lakini hatuitumii na hivyo kuamua kuwauzia raia hao ardhi. Ukitaka ujue ardhi ya nchi hii ina wenyewe, jitwalie tu hata ekari moja ambayo unadhani haitumiwi halafu subiri watakaoibuka. Ukweli ni kwamba ardhi ya Tanzania yote ina matumizi. Isipokuwa matuymizi hayo hayajaingizwa kwenye mfumo unaotambulika kisheria. Wanaoitumia wanajua nini wanachokipata kutoka huko. Maisha yao yanategemea hayo matumizi. Ni vizuri serikali ikitaka kuuza ardhi ikawakutanisha wananchi wote wa eneo hilo na kukubaliana nao kwanza.

    ReplyDelete
  3. Sasa mtu anauziwa mpaka njia, kweli nchi imebaki mifupa.

    ReplyDelete
  4. hivi ni kwanini siku hizi bongo kuna migogogro ya ardhi na hawa raia wa nje????? hawa watu wa ardhi especially mama Tibaijuka tunaomba aishughulikie haraka manake tukichoka zaidi itakuwa kama Libya

    ReplyDelete
  5. Hii itakuwa nchi tope

    ReplyDelete
  6. Yani utafikiri hatuna SERIKALI inauma sana. kwanini wasiuziwe ardhi polini wanakuja kwenye vijiji?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...