ASSAALAM ALAIKUM ANKAL,HONGERA KWA SWAUMU. MAANA SI POLE KAMA WENGI WADHANIAVYO.MFUNGAJI HUFUTIWA DHAMBI ZOTE BAADA YA MFUNGO. SASA VIPI IWE POLE?AMMA BAADU.JAMANI NINA SHIDA YA KUOA MKE WA PILI.MIMI NI MWISLAM WA MIAKA 51. NINA WATOTO 6.WA KWANZA ANA MIAKA 24.WA MWISHO ANA MIEZI 2.KWA VILE MWENYEZI MUNGU KAKATAZA ZINAA,MIMI NAOGOPA HUO UZINZI.NAOMBA WANA LIBENEKE WANITAFUTIE MCHUMBA KWA MASHARTI YAFUATAYO:
1.AKUBALI KUUFUATA USLAM KIKAMILIFU IKIWEMO 
KUSWALI SWALA 5 KWA SIKU.
2.KUPIMA V.V.U
3.AWE CHINI YA MIAKA 30
MWENYE NGUVU KIUCHUMI ATAFIKIRIWA KWANZA(frankly speaking-uchumi wangu ni mdogo)
MAOMBI YATUMWE KWA E-MAIL HII(wjulaibib@yahoo.com}
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Masharti magumu sana ndugu yangu. Ni bora kama utakubali abaki na dini yake.

    ReplyDelete
  2. Nimelipenda ilo sharti la nne

    ReplyDelete
  3. Je mke ulienae ana miaka mingapi na uwezo wake kiuchumi ukoje? Kuhusu VVU itabidi wewe,mke wa sasa na mtarajiwa mpime VVU

    ReplyDelete
  4. Huo ni unzizi unakusumbua kwa sababu huna uwezo wa kuoa mke wa pili! una mawazo finyu...mwanmke akiwa na uwezo wa kiuchumi hawezi kutafuta mwanaume maskini kama wewe.Lea familia yako...

    ReplyDelete
  5. mtu mwenyewe uchumi mdogo watoto team ya mpira halafu unaleta masharti meengi. mie uchumi wangu mnono, but lazina ubatizwe. kwanza mkeo kafanyeje?

    ReplyDelete
  6. kwa hiyo unatafuta mtu wa kushushia matatizo yako? kila la kheri

    ReplyDelete
  7. WACHA UHARIBIFU TAFADHALI TAFUTA MZEE MWENZAKO HAO WADOGO WAACHIE VIJANA SAIZI YAO.

    ReplyDelete
  8. Sharti la kuoa ni lazima uwe na uwezo wa kumuhudumia mke kwa hali na mali.

    ReplyDelete
  9. Kama uchumi wako mdogo mke wa pili wa nini, uislamu sio kuswali tu kama unavyotaka huyo mke wa pili awe, kwanza wewe uwe mwislamu kikamilifu, unataka kuoa wakati huna uchumi na una familia kubwa, si utamyanyasa huyo mke mdogo au ndio unataka utumie pesa zake, umesikia wapi kwenye usilamu jambo hili, mali ya mke ni ya mke, akipenda anaweza kukupa. Kwa maoni yangu hufai kupewa mke, kwanza utamuweza mke miaka 30 na wewe uko dakika za majeruhi, ukija kuzaa nae uwache mayatima.

    ReplyDelete
  10. Wewe ni njaa tu. Miaka 51 unapenda kuoa chini ya 30. Una matatizo....nenda upate ushauri nasaha

    ReplyDelete
  11. mimi uchumi si tatizo kipato changu cha mwezi ni shilingi milioni 6.5, ila ni MKRISTO kama uko tayari, twende kazi, ingawa umri wangu ni 36 na wewe utnataka vitoto vidogo vya watu, badala ya kuchukua mzee mwenzio. Tena wewe unaonekana si mwislam safi maana uislam unataka uoe mke wa pili na kuendelea wenye mahitaji kama vile wajane na wasio na uwezo sasa wewe funga yako haina swiii kabisaaaaaaaaaa unatamaa ndugu yangu. hiyo si dini ni UFISADI wako unakusumbua bora ukazini tu ieleweke kuliko dhambi hii ya dhuluma kwa wasichana wadogo unaotaka kuoa. waachie vijana wenzao nao wafaidi loooooooooooool!

    ReplyDelete
  12. we lazima ni FATAKI tu!

    ReplyDelete
  13. Baba, si uoe huyo mwenye mwana wa miezi miwili? Yaani kweli maisha ni safari, ila hii yako duu!

    ReplyDelete
  14. Wewe unatafuta mke au mtu wa kukulipa pensheni? Suruali ulizivaa ukiwa na nani na sasa unataka kuwavalia watoto wa wenzako misuli!

    ReplyDelete
  15. mwezi mtukufu unawaza uzinzi tu, mweheshimu huyo mkeo uliyenae. pia mtunze kwa kipato chako hicho kidogo, sasa unataka eti mwenye nguvu kiuchumi ili uzitumie? kumbe unapenda mali siyo mke

    ReplyDelete
  16. wewe mwanaume una matatizo. Unaweza tupa sababu za kukufanya uoe mke wa pili? maana watoto unao tayari,tena wa kutosha!! halafu unasema uwezo wako mdogo,sasa mke wa pili wa nini? unatakiwa ukioa mke wa pili umuhudumie kila kitu bila ya mke mkubwa kupungukiwa kwa chochote,wote uwahudumie sawa,hao watoto wako wanapata huduma zote bila mapungufu? nina wasiwasi unazini wewe!!!

    ReplyDelete
  17. Tapeli huyo analolote anatafuta mwenye pesa siyo kuoa

    ReplyDelete
  18. POLE NDUGU WEWE UNATAFUTA MKE AU MALI???? KAFIE MBELE HUKO KAA NA MKEO ULIYENAYE UMEMZALISHA KAMA PAYA.

    ReplyDelete
  19. Hive wewe baba una akili timamu kweli? eti nataka kuongeza mke huyo uliye nafikiri hata hajui senti tano yako badala ya kufiklia hao waliopo watasomaje unawaza mke NENDA WARD YA KICHAA WEWE SIO MZIMA.....................................................

    ReplyDelete
  20. Baba wewe unatuaibisha sisi vijana wenzako wa zamani. Una watoto 6 na kwa umri wao wote wanakutegemea, halafu unataka kuongeza mke wa pili! Huyo mtoto wa mwisho wa miezi 2 inaonyesha bado mama kazi anaiweza.

    Kwanza dini haikuruhusu kwani mwenyewe umesema huna uwezo wa kiuchumi. Yaani hata uzazi wa mpango haukuwapitikia wajameni!

    Sasa na huyo mke wa pili unayemtaka ambaye ni kijana ni lazima na yeye atataka apate watoto wake, jee umepanga kuwa na team ya mpira?

    Wacha hizo fikra mgando kaa vyema na mke wako musaidiane kulea watoto kwa hicho kidogo mutachokipata. Mwenyezi Mungu akiwafungulia milango ya kheri mutafaidika pamoja.

    ReplyDelete
  21. Huyo mke uliyenaye anajua kwamba unataka kuoa mke wa pili?na umwembia kwamba utamtafuta kupitia Blog ya Ankali? kama hujafanya hivyo,ni dhambi inayokuongoza na kukusumbua.Subiri mfungo mwingine ujao utubu kwani huu umechelewa.Na kama anajua,je amekubaliana na wewe?Nina mashaka kama anajua na amekubaliana na wewe.Huu pia ni uvunjifu wa misingi ya imani ya Kiislamu.Tafadhali ondoa wazo hili na umurudie Alhaa ipasavyo.

    ReplyDelete
  22. Ujana wako umekula na wengine hadi umemaliza, sasa unataka uzee wako utafute mtoto wa kumalizia nae, ili akuvishe, akulishe wewe na hiyo timu yako nyumbani lol...eti mwislamu safi..utakuwa wewe???? umeingia choo cha kike babu, nakushauri tafuta sponsor wa kulea hiyo timu yako ya mpira....MKE WA PILI KIZAMANI...

    ReplyDelete
  23. huyu baba anaetafuta mke wa pili mimi nadhani akili zake haziko sawa kwanza yake na huyu mke wake nawatoto 6 bado ni mgogoro hanakipato cha maana kama alivyosema bado anataka kuongeza mke wa pili badala angefikiria jinsi ya kulelea hawo watoto na jinsi ya kuwasomesha ili baaday waweze kujitegemea yeye anawaza kuongeza mke wa pili tena kibaya zaidi ni kwamba anataka mwanamke kijana na mwenye kipato sijui ni taaira gani atakubaliana na huu upuuzi wake eti msichana anakipato chake kizuri na ujana wake aache kuolewa na vijana wenzake aende kuolewa na mzee mwenye familia yake na asiye na kipato ya uwakika labda atafuete kichaa asiye na akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...