Pichani kulia ni Mwanaharakati na muelimishaji wa masuala mbalimbali ya Kijamii yakiwemo ya watoto,Mama Sadaka Gandi akishirikiana na Kampuni ya Prime Time Promotions wakijumuika pamoja na watoto wa kituo cha kulelea  watoto yatima wapatao 75 kiitwacho Mwana Orphan Center,kilichpo Vingunguti jijini Dar jioni ya leo kwa ajili ya futari walioiandaa maalum kwa watoto hao.
Watoto wa kituo cha Mwana Orphan Center wakipata futari pamoja jioni ya leo.Aidha kituo hicho kina jumla ya watoto wapatao 75 ( wa kike 35 na kiume 40).Blog ya Jiachie pia ilialikwa kwenye futari hiyo jioni ya leo,lakini pia ilibahatika  kuzungumza na mlezi wa kituo hicho aitwaye Dada Umi,alisema kuwa kituo hicho kinahitaji msaada mkubwa wa vitu mbalimbali vya shule yakiwemo,madaftari,pia aliongeza kuwa wanahitaji Magodoro kwani waliyonayo yamekwisha chakaa,Vyakula pamoja na msaada wa huduma ya matibabu kwa namna moja ama nyingine..

"Kikubwa zaidi tunaomba msaada wa tupatiwe jenerata kwa ajili ya kusukumia maji kwenye matanki yetu tunayohifadhia maji,ambao ndio mradi wetu mkubwa tunaoutegemea,unaotuingizia fedha kiasi kwa ajili ya kujikimu,kwa sababu maji hayo tunawauzia watu wanaotuzunguka kwenye kituo hiki,ambao ni wengi sana",alisema Dada Umi ambaye amedumu kwenye kituo hicho kwa muda wa miaka nane mpaka sasa.
Mmoja wa wasimamizi wa watoto wa kituo hicho akisaidia kugawa futari kwa watoto hao walioonekana kuchangamka kupita kiasi.
Mama Sadaka Gandi (kulia) pamoja na baadhi ya marafiki zake wakiandaa futari kwa ajili ya watoto waishio katika kituo cha kulelea  watoto yatima wapatao 75 kiitwacho Mwana Orphan Center,kilichopo Vingunguti jijini Dar jioni ya leo.Futari hiyo iliandaliwa na kampuni ya Prime Time promotions ikishirikiana na Mwanaharakati, mama sadaka gandi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kufuturisha deal siku hizi. Kila mtu yupo busy kufuturisha.

    ReplyDelete
  2. Ankal Samahani naomba msaada kidogo maana mimi ni Mkristo, lakini nataka kujua naona makampuni, serikali na watu binafsi wanafuturisha watoto yatima Moja hawa watoto yatima wanatakiwa kufunga pia? Pili mbona kipindi kisichokua cha mwezi mtukufu huwa hatuwaajali hawa watoto ya tima kwa kuwapa chakula kama hv? Mimi ningependa nipate ufafanuzi tu wala sina nia ya kuchafua hali ya hewa. USHAURI ingekua ni bora tungewajali pia wakati wa siku za kawaida ingekua vizuri zaidi.

    ReplyDelete
  3. Nadhani ni moyo wa kutoa na kulisha wasiokuwa na uwezo kama dini zote zinavyosema.
    Kwenye mwezi huu kuna wafungaji wanashindwa hata kupata futari kwa sababu ya ugumu wa maisha unaosababishwa na viongozi wao kudhulumu mali za taifa kwa faida zao binafsi.
    Kwa kufanya kwenye mwezi huu basi kunatupa urahisi wa kufanya hivyo hata miezi mingine, point hapa ni kusaidiana, aliye na kiasi kumsaidia asiye nacho kabisa.
    Munu awaongezee wote wenye kujitolea kusaidia wasiojiweza.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana kutoa ni moyo na si utajili endelea kutoa msaada hata mwezi mtukufu ukiisha mwenyezi mungu atawazidishia wale wote wanaojitolea

    ReplyDelete
  5. Hongera sana endelea kutoa hata mwezi mtukufu ukiisha mwenyezi mungu atawazidishia wale wote wanaojitolea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...