![]() |
| Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Rajabu Kiravu. |
Na Mwandishi Wetu.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Igunga, baada ya kupokea Barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi, pamoja na chaguzi ndogo za madiwani kwenye kata 22 katika halmashauri mbalimbali.
Katika Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga utafanyika kuanzia tarehe Septemba 6, 2011, huku Kampeni zikitangazwa kuanza Septemba 7 mwaka huu hadi Oktoba 1,2011 huku siku ya kupiga kura ikiwa imepangwa kuwa Oktoba 2.
Aidha taarifa hiyo ya Tume ya Uchaguzi imeongeza kuwa, madaftari ya wapiga kura yatakuwa wazi katika vituo vya wapiga kura waliojiandikisha kuanzia septemba 22 ambapo zoezi la kuhakiki litafanyika kwa wiki moja.
Wakati huo huo Tume imetangaza kufanyika kwa chaguzi ndogo za madiwani katika kata ambazo viti viko wazi kutokana na sababu mbalimbali ama za kujiuzulu ama kufariki kwa madiwani.
Uteuzi wa wagombea utafanyika septemba 9 huku kampeni zikitarajiwa kuanza tarehe septemba 10 hadi Oktoba 1.
Tume imewataka wananchi wote pamoja na vyama vya siasa kufuata ratiba na taratibu iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia siku ya Uteuzi hadi Kupiga kura ili kutimiza haki zao za kikatiba za kuchagua viongozi wanaowataka.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...