Usu Mallya Diana Mwiru
 Mtandao wa Jinsia Tanzania ni mmiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998, Kiwanja namba 22/3/1 lililoko katika eneo la Mabibo Dar es Salaam.
Mtandao wa Jinsia ulinunua jengo hilo kutoka kwa Mfilisi (Benki ya Rasilimali Tanzania- TIB) kwa Iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited ambayo ilikuwa sehemu ya kampuni tanzu ya Tanzania Textile Company Limited (TEXCO) kwa gharama ya shilingi milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15/6/ 1997.
Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikuwa wa wazi uliotangazwa katika vyombo vya habari nchini hususan magazeti.
Baadhi ya watumiaji wa ofisi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakati TEXCO ikiwa inafilisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio. Baada ya TGNP kushinda tender, baadhi ya watumiaji hao , mnano mwezi wa Julai 1997 walifungua kesi namba 215 / 1997 dhidi ya TIB kama mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pili katika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka kumi na mbili mpaka kufikia tarehe 15/10/ 2009,uamuzi wa Mahakama Kuu ulipotolewa. na Mheshimiwa Jaji T.B Mihayo wa mahakama kuu hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama.
Wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu ukiendelea, mnano tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika Mahakama ya Rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu ya kutowatoa kwenye jengo kwa kupitia ombi na 129 la 2009 ombi lao limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa tarehe 23 /8/2011.
MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA
TGNP wamiliki halali wa hili jengo tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyotolewa terehe 23/8/2011. Tutaendelea kuwataarifumaendeleo ya mchakato huu.

Usu Mallya Diana Mwiru
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WA Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...