Waziri Mkuu wa Serikali ya chuo kikuu cha TIBA ( IMTU) Daniel Msafiri akisistiza jambo Aug 25-2011 mbele ya waandishi wa habari  wakati Viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha TIBA (IMTUSO) walipokutana na waandishi wa habari na kuzungumza nao kuhusu matatizo mbalimbali ya kitaaluma yanayoendelea kuwakabili wanafunzi wa chuo hicho, (kushoto mwanamke) ni Waziri wa Afya wa Serikali  ya wanafunzi IMTU Vivian Mpangalala
 Rais mstaafu wa chuo Kikuu cha TIBA cha IMTU Jonas Mushi akionyesha baadhi za nyaraka za Mikataba  ya chuo na wanafunzi wakati viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha TIBA (IMTUSO) walipokutana  na waandishi wa habari kuzungumzia matatizo mbalimbali ya kitaaluma yanayoendelea kukabili wanafunzi wa chuo hicho, Mwengine ni Waziri Mkuu wa Serikali ya chuo kikuu cha TIBA (IMTU )Daniel Msafiri (suti nyeusi), (Aug, 25,2011) jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Elimu wa serikali ya wanafunzi wa IMTU cha mjini Dar es Salaam Mwita Waibe
 (kulia) akionyesho nyaraka kwa waandishi wa habari inayohusu makubaliano ya tiba chuoni hapo baina ya uongozi wa chuo cha IMTU na Wanafunzi  August 25,2011 jijini.  Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha TIBA (IMTUSO) imekutana na  wanahabari hao kuzungumzia matatizo  mbalimbali  ya kitaaluma yanayoendelea kuwakabili wanafunzi wa chuo hicho (kushoto pichani ni ) Waziri Mkuu wa Serikali ya ya wanafunzi wa IMTU Farah Ibrahim
Rais wa  Serikali ya wanafunzi wa chuo cha TIBA (IMTU) cha jijini Dar es Salaam Yeredi Chacha (suti nyeusi) akiongea  jijini Dar es Salaam Aug,25,2011 katika mkutano wa viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha TIBA (IMTUSO)  kuzungumzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wanafunzi wa chuoni hapo mbele ya waandishi wa habari, (Kulia mwenye miwani ) ni Rais Msataafu wa chuo hicho  Jonas Mushi. 
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Habari ya kazi kaka michuzi.
    Samahani kwa hili,naomba kupitia kona hii ya maoni niwasiliane kwa kina na Rais wa chuo anayeongea hapo Bwana Yeredi Chacha.Kama atabahatika kusoma hapa au kama anaweza kupewa taarifa na mdau yeyote atakae pata hii taarifa.Naomba niwasiliane nae kwa mail address: joachim.kulwa@yahoo.com au simu no.+91 8712744965.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...