Ankal, nakutakia sikukuu njema ya Idd wewe, 
familia yako na wadau wote wa blogu ya jamii.
Ni kuwajuza tuu kuwa hapa Sauzi sikukuu za kiislamu kama Idd El Fitr, Idd El Haj na Maulid hazijajumuishwa kwenye sikukuu za kitaifa. Ni kama leo, tupo kwa job tunawajabika.Yaani kwa kifupi, shule na ofisi zote za serikali na binafsi shughuli zinaendelea kama kawaida.
Ila kwa wale waislamu, wanaruhusiwa kutokufika kwa ofisi na wakaendelea kusherehekea kwa namna zao, mfano hapa job kwangu waislamu hawajafika kazini leo.

Mdau, John
Eastern Cape, Sauzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MDAU JOHN UPO SAWA KABISA HAPA SOUTH AFRICA SIKUKUU ZA KIISLAMU HAZITAMBULIKI KITAIFA NA HATA UISLAM HAUTAMBULIKI SANA WANACHOJUA NI KUWA LEO NI X-MAS YA WAHINDI ILA SISI TUSIOKUWA WAISLAMU TUNAWAHESHIMU WAISLAM KWA KUWA NCHI TUNAZOTOKA TUNAAMINI KILA MTU ANA HAKI YA ANACHOKIABUDU BABA WA TAIFA KAMBARAGE NYERERE NAMSIFU KWA KUTOTUGAWA KWA MATABAKA YA DINI WALA MAKABILA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU JK NYERERE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
    MDAU SAFARINI TRIPOLI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...