Rajab Mhamila "Super D"
Na Mwandishi Wetu

Kocha maarufu wa mchezo wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila 'SUPER D' aliyeamua kutumia njia ya DVD kuwafundisha watu mbalimbali kujua na kutambua sheria za mchezo huo ameachia kazi nyingine tatu mpya.

Kazi hizo tatu zinausisha mapambano kadhaa ya nyota na mabingwa wa ngumi za kulipwa Duniani, ziliachiwa sokoni zaidi ya wiki moja sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa 'clips' za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.

''katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tatu tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition '' alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.


Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza 'live' chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naomba kuuliza hivi kina Stanley Mabesi(mtoto wa msasani mikoroshini) na yule Mzambia James somebody wapo wapi siku hizi? Nakumbuka wakati nipo msingi Mabesi na yule mzambia walikuwa rivals sana. Kuna anayejua walipo?
    *** Habib kinyogoli na Abdallah Kibadeni ni ma-legend wa michezo Tanzania. Wanahitaji kupewa tuzo ya kitaifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...