Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Poleni sana wadau wa ughaibuni na nimefurahishwa na uwazi wenu kuwa wengi wenu mnatumia uraia wa nchi mbali mbali ili kuweza kumudu maisha. Pia nakupongezeni tena kwa kuweza kumstiri mwenzenu ambaye ametangulia mbele ya haki. Na hii pia iwe fundisho kwa wengine wanaofikiri kwa vile wameshapata karatasi ndio mambo yamekwisha na kukimbia wenzao ambao ndio kwanza wanawasili ughaibuni. Leo uhai kesho mauti. Sisi WaTZ tunategemea kifamilia, kijirani, ki-kijiji, ki-mtaa, kikazi, na kitaifa. Mimi kabla sijakaa sana na wazungu nilifikiri hawa watu hawasaidiani. Kumbe bwana hawa wazungu wanasaidia tena sana na wanajuana popote pale walipo na serikali yao ipotayari wakati wowote kupeleka jeshi kumuokoa mtu mmoja. Tena nawapa pole wafiwa. Mungu amlaze pema peponi marehemu.

    ReplyDelete
  2. hili linaeleweka kabisa. Kuna waheshimiwa wako serikalini watoto wao wamejiripua Kisomali na wanafaidi haki zote za wakimbizi wa kisomali. Tena ni wakristo, inabidi waishi maisha ya kiislamu na kisomali. Maana Serikali ya uingereza inafuatilia sana maisha yao hao wakimbizi. Mpaka akipata utambulisho ndio wengine wanarudia majina yao ya zamani na maisha yao ya zamani. Lakini maiti ya mtanzania huwezi kuupeleka Somalia.

    ReplyDelete
  3. Nimeguswa sana na uungwana wa hali ya juu mliouonyesha. Nafahamu uhamiaji ni watu waelewa sana na watawajibu kiungwana.
    Hii inatupa tulioko Tanzania kwenye migao ya kila kitu picha nzuri ya watanzania wenzetu walioko ughaibuni

    ReplyDelete
  4. Siku ingine msirudie pitieni ubalozini mkiona vigumu zikeni huko huko. Watu wanatumia maiti kusafirishia madawa ya kulevya.Maiti zinapasuliwa zinawekwa madawa ya kulevya zinashonwa na kuwekwa kwenye majeneza kama ilivyotokea mkasa ule wa maiti iliyodakwa mbeya ikitokea zambia kama sijakosea na vyombo vya habari vilitangaza sana Tanzania maiti kutumiwa kama begi la kusafirishia madawa ya kulevya toka mataifa mengine.

    Sababu zenu za msingi lakini mjue na uhamiaji wamejitahidi.Ingekuwa hawana huruma ingerudishwa hiyo maiti ugiriki na hakuna ambaye angewalaumu.Mnapotoa taarifa ubalozini wao wanajua cha kufanya kiuhamiaji n.k.

    Hata kama makaratasi yana matatizo wana wanasheria wanajua nini kiwe nini.Pia hata mtu ukijilipua na kukana uraia vizuri utoe taarifa ubalozini ili ukijisikia kurudi kuzikwa kwa Tanzania kwa nduguzo isiwe taabu.Mbona tuna watanzania waliozikwa kanada kwa ndugu zao wakati wana uraia wa Tanzania.Hata ukikana uraia ripoti ubalozini au uhamiaji.

    ReplyDelete
  5. Kubalini tu ndugu zangu mlivunja sheria. Mtu ana uraia wa nchi nyingine ninyi mnamleta tanzania. Je hao wenye nchi wakiamua kumtafuta mtu wao mtamfukua?

    ReplyDelete
  6. tanzania imefika wakati wa kuwa uraia wa nchi mbili...

    ReplyDelete
  7. There was a noted debate regarding Dual citizenship last year and i believe 2009 too. Wonder what happened, its all gone quiet. From this discussion there was an impression that the governement had in principle agreed to go ahead and legitimize Dual citizenship for Tanzanians. Anyone with an idea on this issue, imeishia wapi?

    ReplyDelete
  8. Wafiwa poleni sana na Uhamiaji mmefanya jambo jema kuelewa kwani naelewa suala kama hilo ni suala gumu mno. Nadhani kama suala la 'Dual Citizenship' lingekuwepo kusingetokea matatizo mengi ya namna hii.Kwa viongozi wetu mnaohusika kama mnasoma blog hii; Suala la watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili limefia wapi???? Maana tumekuwa tukidanganywa hasa kwenye 'Diaspora' takriban miaka mitatu mfululizo kuwa mpaka kufikia mwishoni mwa waka jana lingekuwa limekamilika. Sishangai sana kama 'wadau' wameshaanza kususia 'Diaspora meetings' kwa kuwa wanaona ni 'waste of time' kama suala muhimu kama hilo linalomgusa kila Diaspora linakuwa magumashi tu. Nasikia suala hilo la 'Dual Citizenship' limesitishwa 'pending' suala la muungano, je ni kweli?? Na kuna minong'ono kwa wadau wa Diaspora kuwa sisi tuliopo nyumbani ambao tumeridhika na uraia wetu mmoja, tunaogopa kuwapa waliopo ughaibuni uraia wa nchi mbili maana tupo 'naive' (kwani inferior ni strong word), kwa kuogopa watakuja kuingia kwenye siasa, private & public companies na hivyo 'watatupiku' na nafasi zetu zitakuwa 'redundant', je ni kweli? Sasa badala ya kuwapa 'Dual Citizenship' hawa Diaspora wetu ili waje watuelimishe na kuendeleza nchi yetu kama walivyofanya watani wetu wa jadi ambao hata ukiangalia 'remittance' zao nchini kwao zinatisha kutokana na faida ya kuwa na raia mbili, sisi tunakuwa tuna sua sua kwa sababu ambazo hazina msingi.Hebu viongozi wetu 'at least for once, let's get serious because it's beyong beggars belief' kuwa suala hilo limechukua muda wote huu pamoja na kuwa 'legal experts' wa kumwaga hapa nchini.

    ReplyDelete
  9. Jamani hii mbona mie najua mtu mmarekani aliletwa kuzikwa hapo Tanzania? Sheria inasemaje? hebu tupeni darasa.

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli huyu muandishi ni Mtanzania,na hata kama hana Pasipoti,basi Uhamiaji uchukue UTARATIBU wa kumpatia hiyo document muhimu kwa jina atakalo yeye hata kama hilo alilotumia hapo ku-saini sio lililopo katika Pasi yake yakusafiria. Maelezo kwa ufasaha katika lugha ya Kiswahili ndio jambo kubwa la kuzingatia katika DIASPORA.Ahsanteni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...