Basi la Abiria lililokuwa likikitokea Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaam,likipita kando ya Barabara ya Kilwa katika kipande cha Nyamwage mpaka Somanga ambacho kiko kwenye matengenezo kwa hivi sasa.
Moja ya madaraja yanayojengwa katika barabara itengenezwayo hivi sasa ya Nyamwage mpaka Somanga likionekana katika hatua nzuri za matengenezo yake.
Sehemu ya Barabara iliyokuwa tayari imewekwa lami,ikiwa imezibwa kwa gogo la mti ili kuzuia magari yasipite kwani bado iko matika matengenezo.
Baadhi ya Wataalam wa ujenzi wa barabara kutokea Nangurukuru kuelekea Lingaula mpaka Ukuli,mkoani Lindi wakiwajibika mchana wa leo.
Kipande ambacho kiko kwenye matengenezo cha Nangurukuru mpaka Lingaula.
Wataalam wa ujenzi wa Barabara ya Nyamwage mpaka Somanga mkoani Lindi wakiwa katika shunguli ya ujenzi wa barabara hiyo.
Gari la Wakandarasi wa ujenzi wa barabara ya Lindi likipita katika sehemu iliyotengenezwa maalum kwa kupita magari ili kupisha ujenzi wa barabara ya Nyamwage mpaka Somanga.
asante kwa kazi nzuri sana hiyo ni moja ya maendeleo yaliyo chelewa tangu tupate uhuru wananchi wa kusini tumevumilia sana
ReplyDeleteKweli inabidi tushukuru hata kwa hili,maana imefikia hata kupata huduma muhimu inakuwa ni kama upendeleo(favour) kumbe ni haki yetu kama zilivyo haki nyingine kama maji,umeme,shule ,hosptali,madawati,nk.
ReplyDeleteKujengwa kwa barbara ni moja ya hatua kubwa za kuleta maendeleo lakini imechukua mda mrefu sana kufikia hapa,yote hii inasababishwa na ubinafsi wa viongozi wetu wa kujipendelea wao na familia zao.
Mungu ibariki Tanganyika.