Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Dar es Salaam leo August 26,2011 limetoa taarifa ya kuwaalika waislam wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika swala ya IDD- El- FITR inayotarajiwa kuswaliwa siku ya Jumanne 30 Aug au Jumatano 31 Aug,2011 kutegemea na Muaandamo wa mwezi katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Pichani Skeikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Salum akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari alipokutana nao leo, (kulia) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkoa Dar es Salaam (BAKWATA) Sheikh Said Ponda na (kushoto ) Mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Shukuru Kilakala. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO),

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. assalaam aleykum ankali wallah mi najickia faraja sana nikimuona USTAADH ALHAD SALUM yan nakumbuka enzi zile ananifundisha alifu chuoni kwake al MADRASAT L MAAMUR mungu amzidishie inshaallah amlipe kwa kila khery anazofanya na amuongoze katika mambo yake aaaamiin....!
    muddy programmer
    udom(informatics)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...