Wanahabari wa kutoka vyombio mbalimbali wakiwa kazini ndani ya Bunge Dodoma
 Wanahabari wakifuatilia hotuba na mijadala bungeni
 Mpiga picha wa Mwananchi Edwin akiwa kazini
 Wanahabari zaidi
 Kila mtu yuko bize asije akapitwa
 Umakini wa hali ya juu unahitajika
 Mkongwe Mzee Ntabaye akimpa haya na yake chipukizi Alvar Mwakyusa
 Rashid Zahoro wa Uhuru, Basil Msongo wa Habari Leo na Lucas Liganga wa The Citizen ndani ya Nyumba
 Mkurugenzi wa SportsTV ya Dodoma Abdallah Majura (shoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli
Mwanahabari Msami wa TBC1 (Shoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Kondoa Kusini Juma Nkhamia (kulia) na Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika.
---------------------
Kombani- Tundu Lissu mchochezi

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Celina Kombani amesema bungeni kuwa, Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Tundu Lissu ni Mchochezi na anawapotosha Watanzania.

Kombani amemtuhumu Lissu kuwa, ana usongo na Urais wa Tanzania, na anavuka mipaka katika baadhi ya mambo anayozungumza.

Waziri Kombani amemtuhumu Lissu kwamba amewasilisha bungeni Muswada wa Mabadiliko ya Katiba bila idhini yake, na amemuuliza Spika wa Bunge kama Kanuni za Bunge zinaruhusu mawaziri vivuli kufanya hivyo.

“Avute subira, asubiri wakati wa kuchangia Katiba yake yote ya tumboni yatatoka” amesema Kombani wakati anajibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

“Hatujaanza kujadili Katiba mpya, wakati haujafika” amesema Kombani na kusisitiza kwamba, Katiba si lelemama, ni sheria mama. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. WANA HABARI BUNGENI MOROGORO?AU DODOMA?KWA UJUMLA HII BLOG INAFANYA KAZI KUBWA NA NZURI,KULINGANISHA NA WINGI WA HABARI MNAZOPKEA KUANDIKA MOROGORO BADALA YA DODOMA KWETU SISI SI TAZTIZO(TUNAELEWA).MICHUZI NA WAFANYAKAZI WAKO MPO JUU SANA..SIJAJUA HUWA MNALALA SAA NGAPI BLOG INAZUNGUKA 24HRS!!BIG UP

    David V

    ReplyDelete
  2. Huyu tundu (what's in a name) lissu noma. Kakaa kigomvi gomvi hivi. Hatumii hekima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...