HII NI ZANZIBAR YA MIAKA HIYO, HAPA NI MTAA WA KISIWANDUI ENEO AMBALO KWASASA NDIPO PALIPO JENGWA OFISI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI, BAHARI HII ILIANZIA MTAA WA MAISARA HADI ILIPO HOTEL YA BWAWANI
JENGO HILI HADI LEO LIPO NA LINATUMIWA KAMA KAWAIDA HAPA NI MTAA WA DARAJANI JENGO LINA ANGALIANA NA MAKONTENA YA DARAJANI LIMEPAKANA NA SOKO KUU LA DARAJANI NA DUKA LA MUZAMIL KUSHOTO KWAKE NA HAPO HASA NDIPO PALIPOKUWAPO NA DARAJA LILILO UNGANISHA KATI YA MJI MKONGWE NA NGAMBO, KUMBUKA KUWA MAJI HAYA YA BAHARI  YALIANZIA MTAA WA MAISARA HADI HOTELI YA BWAWANI NDIO ULIO KUWA MPAKA WA MITAA HIYO MIWILI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Eeeeeeeh umeturudisha mbali sana, enzi za 1920s huko.

    Hongera kwa kuleta picha za historia.

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa kumbukumbu nzuri, lakini hiyo picha hiyo ni wakati Mzee Karume atakuwa na umri wa miaka 5 au hajazaliwa kabisa! - hivyo hizo picha si za wakati wa Mzee Karume ni za zamani zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...