Hali yako kaka,
Nimesoma habari ya kukanushwa kwa kashfa ya Wikileaks dhidi ya JK. Hakika nimeshangaa sana hawa jamaa nilikuwa nawaona Baab’Kubwa kumbe aloso. Nakutumieni email ya huyo mama Pile alietajwa akikanusha na hata kutaka aombwe  radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Hiyo email imesambaa kila mahali.

Unajua kaka, mie niko huku nje kitambo ila naijua picha yote hata kabla sijaondoka hapo Bongo mwaka 2009. Kwa mujibu wa vyanzo sahihi email hii ilitumwa na mtoa habari hapa ambaye mimi naweza hisi ni huyo balozi, mwaka 2006 – yaani mwaka mmoja baada ya serikali ya JK kuingia madarakani. lakini cha kushangaza ni kwamba serikali ya marekani kupitia Rais George W. Bush kipindi kile walichunguza na kujiridhisha kwamba serikali yetu si serikali ya ovyo ovyo kama jinsi tunavyojaribu kujiharibia sisi wenyewe na siasa zetu za maji taka zilizojaa tamaa ya kutaka kuwa viongozi pasi na kuangalia jinsi gani tunaweza litengeneza taifa kwanza.

Rais Bush aliweza hata kuja mwaka 2008, ikiwa ni baada ya zengwe hili kuanza kupikwa. Marekani katu asingeruhusu Rais wake atie mguu Tanzania (na Kulala siku 4! Ambapo ni nadra kwa Africa) kama habari hizo zingekuwa na lepe la ukweli.

Anyway, tukiliacha mbali hio, mambo haya yote ni sehemu ya watu wachache wanaotumia yale yaliyoonekana kipindi hiki ili kumchafua JK (maskini ya Mungu). Kwa kweli ana kazi kubwa huyu bwana mkubwa. Yaani hakuna hata moja ya mazuri lukuki aliyofanya ambayo watu wanapenda yaanikwe. Iko haja nyie wana habari mnaoheshimika na mliobobea mjaribu kumsaidia JK pamoja na Tanzania kwa ujumla. Vinginevyo madudu kama haya yataendelea tu. Ila wajue watakuja kumkumbuka kwani daima msema kweli Mungu humlinda. We ngoja tu.

Tena basi mjue nyie mnaotoa habari za watu kustarehe na kujirusha kila kukicha kwenye blogu zenu mnachukiwa kweli. Hao wenye nia mbaya wanataka kudanganya dunia kwamba Tanzania kuna matatizo, ila nyie mnawashushua san asana maana nchi yenye matatizo watu wasingejirusha kwamwe! Hahahhaa yaani hata mtoto mdogo hadanganyiki.

Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mbona sielewi hii mambo sasa, can someone tell me what is exactly going on here? Tatizo ni balozi?? maadui wa JK?? kambi za urais 2015??? wenye uelewa zaidi watujuze jamani mana hatupendi kusikia rais wetu anahusishwa na mambo ya ajabu kama haya. Mimi binafsi ninazo suti za kutosha, je rais atashindwa kununua suti jamani??

    ReplyDelete
  2. Mdau ametoa wito kwa waandishi wa habari kujaribu kumsaidia JK na Tanzania. Kama unamaanisha kumsaidia JK kwa kuanika ukweli kuhusu watu wanaoharibu nchi kama kina Richmond/Dowans, Meremeta, Dili la Rada, Dili la EPA nk sawa. Kama unamaanisha kumsaidia JK kwa kuwa tu ni maskini wa Mungu unawatafuta lawama waandishi wa habari makini.
    Pia ingekuwa vema utoe na mifano ya mambo mazuri lukuki aliyoyafanya ili kushadidia hoja yako. Hakuna ubaya kuwakumbusha watu.

    ReplyDelete
  3. Nanukuu maneno ya aliyeleta hii mada: "....serikali yetu si serikali ya ovyo ovyo kama jinsi wenyewe tunavyojaribu kujiharibia na siasa zetu za maji taka zilizojaa tamaa ya kutaka kuwa viongozi...."

    Hapa na mimi sielewi mtoa mada ulikuwa unamaanisha nini? Kwani Wikileaks ni wanasiasa wa Tanzania? Mada hii imehusishwa vipi na siasa za Tanzania?

    Ninachoweza kufikiri mimi ni kwamba Marekani ina namna nyingi za kuilinda nchi yake na raia wake. Propaganda ni moja ya mbinu wanzozitumia wanasiasa wengi kupata taarifa ambazo si rahisi kuzipata kwa njia ya kawaida. Walichoandika Wikileaks naweza kukiita ni propaganda. Kumbukeni Marekani na hao jamaa hapo mashariki ya kati haziivi. Na mnajua nchi yetu ni nchi isiyofungamana na upande wowote. Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k. wooote ni marafiki zetu na wote wanaweza kuwa maadui zetu. Hivyo Marekani inapoona tuko karibu na adui yake ni lazima awe na hofu. Mnakumbuka ugaidi uliotokea kwenye balozi za Marekani nchiniTanzania na Kenya? Kama mnasoma vyombo vya habari mtaona kwamba watanzania wamehusishwa katika ugaidi huo. Kwa mtaji huo kuna uwezekano marekani hawatuamini.

    Ninachojua mimi hawa jamaa wanajaribu kuhakikisha kwamba ugomvi wao unasambaa hata kwa nchi zingine. Marekani atataka watu wengine wasimsapoti mwarabu ila yeye, hali kadhalika mwarabu atataka watu wengine wasimsapoti mmarekani ila yeye.

    Kuna njia tatu watakazotumia kuhakikisha wanatuingiza kwenye ugomvi wao:
    1. Dini
    2. Uwekezaji
    3. Misaada

    Kwa vile tuko maskini ni rahisi sana tukaingia mkenge bila kujua kama tunaingia mkenge. Watakaoumia ni sisi wenyewe. Mimi ningeshauri watanzania tulione hili kabla hatujapokea moja wapo kati ya mambo hayo matatu ili tuepukane na uchochezi wowote utakaoletwa na hao jamaa. Tutakaoumia ni sisi wala sio wao.

    Kwa mtaji huo nasema raisi na watanzania wengine tusiwe na wasiwasi hizo ni propaganda tu.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau wa tatu kutoka juu umeandika vizuri sana..Washindwe na walegee. naomba watanzania tushikamane kwa hili na tumuunge mkono rais wetu.Kama alivyosema jamaa hapo juu hawa jamaa wanaweza kutuingiza kwenye ugomvi bwana..Kuna sehemu humu nilitoa comment kwamba watu waache kasumba ya kusema Tanzania haiwezi kuchafuka..inawza kuchafuka hawa jamaa wanakuja kupitia stahili nyingi kama alivyosema hapo juu huyu jamaa au kupitia kwa waasi,vyama vya siasa n.k.KWA SUALA HILI NAOMBA TUWEKE VYAMA VYA SIASA PEMBENI NA KUMSAPOTI RAIS WETU....

    Mungu ibariki Tanzania

    David V

    ReplyDelete
  5. Naungana na mdau wa tatu hapo juu. Kusema kweli kama hatutakuwa na akili tutagombana wenyewe kwa kutekeleza matakwa ya watu wasio na utu kwetu. Hebu angalia ugaidi uliotokea kwenye hizo balozi za Marekani. Waliokufa wengi wao ni waafrika. Na kama kweli waliohusika ni watanzania, mtu unaweza kujiuliza walihusika kwa nia gani? Watanzania tuna ugomvi gani na wamarekani hadi mtu ajitolee kuangamiza balozi zao? Na kama hatuna ugomvi na Wamarekani hao watanzania walitumwa na nani kufanya uhalifu huo? Kuna faida gani ya kumsapoti mtu halafu wanaoumia ni ndugu zako? Ni kweli mambo matatu aliyotaja mdau hapo juu yanawezatumika kutekeleza matakwa ya hao wazito. Tuangalie zaidi maslahi ya nchi zetu na watu wetu hasa umoja wetu ambao ndio msingi mkubwa wa maisha yetu. Baadae ndipo tutekeleze matakwa ya hao jamaa kama hayana madhara kwenye umoja wetu.

    ReplyDelete
  6. Huwa najiuliza kwa nini inapotokea rais wetu au nchi yetu kukashifiwa baadhi ya vyombo vya habari vinakuwa mstari wa mbele kushabikia utafikiri wao ni malaika. Hivi ni mhariri gani au mwandishi gani atakayeweza kusimama na kusema yeye ni safi. Ni maovu mangapi mnafanya na hao hao ndio wananunuliwa na mafisadi kuwasafisha na kununuliwa magari ya kifahari. Hebu kuwenu wazalendo. Namsapoti yule aliyesema ana suti kibao, sembuse rais atashindwa kujinunulia suti mpaka akubali kuhongwa? msikurupukie mambo na kumchafua rais. Yote haya yaliyotuhumiwa yaweza kuwa mipango ya kuichafua nchini yetu. Mungu ibariki Tanzania yetu yenye amani. Wanaotaka kuichafua washindwe na walegee.

    ReplyDelete
  7. Hii inafurahisha, kwamba kwa mara ya kwanza nimesoma mada ya wantanzania ambayo haina matusi wala kashfa..ila muono wa mawazo.
    Nadhani nakubaliana na wale wanaosema kuwa JK ana bahati mbaya, kwani mazuri ayafanyayo hayasemwi, mabaya wanamsingizia..mfano tayari kipindi cha kwanza chake waliandika kuwa anapenda kutembela nje. Hiyo ni kashifa kama ya suti tano, kwamba mtu aliyewahi kuwa waziri wa mabo ya nje, kawa na safari za nje kibao, leo hii ataona ameukata kuwa rahisi ndiyo nafasi ya kwenda nje? alijibu tuhuma hizo.
    Haya sasa tunaambiwa aliletwa Londono kununuliwa suti tano! Mdau wa kwanza hapo juu ameeleza bayana, kuwa wengi tunaweza kununua suit hizo tano bila shida, sasa kama rahisi wa nchi analinganishwa hivyo, kuwa kivutio kwake ni suti, na nauli bure kuja Ulaya, ni kashfa. wdau wengi jana pia walisema, ingekuwa bora, ama kuwanaymazia hawa jamaa( balozi) au kumshataki kwa kashafa( mwana sheria mkuu.
    uzushi na upuuzi kama huu unachukua muda wa watanzania na wengineo bila msingi.
    Ni kukashifu watanzania na rahisi wao, kuwa, kama rahisi anaweza hongwa suti tano, je mtanzania wa kawaida, si hata pipi inatosha?

    ReplyDelete
  8. wanasiasa na viongozi wa dini mna jukumu kubwa sana kuhakikisha mambo aliyotaja mdau hapo juu hayaleti mushkeli kwenye nchi yetu kwani ninyi ndio mpo mlangoni. Hao jamaa hawawezi wakaingia chumbani kabla hawajaonana na ninyi.

    ReplyDelete
  9. Wako wanaofikiri kuwa kila kinachoandikwa kwenye wikileak basi ni ukweli kama uliomo kwenye vitabu vya dini. Wakati hao ni watu wenye maslahi yao na wanaweza kufanya chochote kulinda maslahi yao. Wanaweza kusema uwongo vile vile, kingine hata huyo balozi anaweza kutunga uwongo. Of all the things suti? Yaani suti hizi hizi za kuvaa? balozi mzima anakaa kitako kuandika upuuzi kama huu? Kweli akutukanae hakuchagulii tusi maana ametuona Watanzania masikini sana mpaka tunawaomba waarabu wamnunulie rais wetu suti. Kwa kweli najua watu wao wanasoma humu, tunataka tuombwe radhi kama taifa kwa kututukana matusi ya reja reja. Na huyo balozi asiruhusiwe tena kukanyaga nchini mwetu hata kuja kutalii tu, anafuata nini na sisi ni masikini hata nguo za kuvaa rais wetu zinamshinda? Akae huko huko kwao!

    ReplyDelete
  10. Na kubaliana kuwa Amerika na alliances wenzake wanaongoza kwa kufitinisha kwa kutumia njia kadha wa kadha kwa maslahi ya nchi zao ila sio kila kinachomgusa Rais huwa sio kweli na linapomgusa mnyonge iwe ndio twamuoshea vinywa na kelele kibao. Yapaswa kuelewa Rais ni kiongozi aliyezungukwa na mabausa wa nguvu zote na propaganda za kila aina na hawa wanamajukumu ya kumlinda kiongozi kwa jambo lolote na hasa kwa utamaduni huu wa mtazania kulindana madarakani zaidi kwa cheo cha Rais.

    Sio busara kuamini moja kwa moja ila kupima na kuchakachua ndio kigezo cha msingi zaidi. Kimsingi binaadamu wote ni sawa na tuwepesi kutenda makosa ama kwa tamaa au kuteleza na baadae pakishatoboka mbio hukimbilia kuziba au kuweka viraka. Kwani hata ukitenda kosa na kufikishwa mahkamani unakataa kwa kuamini kuwa ipo siku utashinda kesi.

    Sitaki nichangie mengi ila hakuna aliyemsafi kwani unaweza tenda kosa dogo ama kubwa ukadhani hakuna atayeliona ila siku ikifika mambo hadharani. Naomba tuchambue na kupima na sio sote tukimbilie kuweka kifua mbele ati ni dowa kwa Rais na watu wake na Tanzania kwa jumla. Watanzani jitambueni na kujielewa

    Nawakilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...