Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Mohamed Babu,akikata utepe wa wakati wa uzinduzi wa bustani ya mzunguko wa ulioko karibu na stendi kuu ya mabasi ya Bukoba iliyotengenezwa kwa ufadhili wa kiwanda cha samaki cha VicFish kilichoko mkoani Kagera kwa zaidi ya shilingi milioni 27 , uzinduzi huo ulifanyika jana, kushoto kwake mwenye tai ni meneja mkuu wa kiwanda cha hicho Nurdin Salim na kulia kwa mkuu wa mkoa ni Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila.
Mkuu wa mkoa Mh Mohamed Babu akizindua bustani ya mzunguko ulioko kribu na stand kuu ya mabasi ya mabasi ya Bukoba.
Mkuu wa mkoa akiwa mbele ya sanamu ya mgomba iliyotengenezwa kwa rasilimali mbalimbali iliyoko katikati ya bustani ya mzunguko uliko standi kuu ya mabasi, kutoka kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba Khamis Kaputa, katibu tawala wa mkoa Nassor Mnambila na kulia kwa Babu ni meneja mkuu wa kiwanda cha samaki cha vicfish Nurdin Salim.
Picha na Habari Na Audax Mutiganzi, Globu ya Jamii, Bukoba MKUU wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu amewashauri wawekezaji hapa nchini kutumia sehemu ya faida wanayoipata ambayo inayotokana na shughuli mbalimbali za uwekezaji wanazozifanya katika kuisadia jamii. Babu alitoa ushauri huo jana kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa bustani ya iliyopo katika mzunguko iliopo karibu na standi kuu ya Bukoba wenye sanamu ya mgomba na maporomoko ya maji iliyoko ndani ya manispaa ya Bukoba iliyotengenezwa na hisani ya kiwanda cha samaki cha VicFish kwa zaidi ya shilingi milioni 27. Alisema wawekezaji wanapoisadia jamii wanakuwa wanajijengea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kuwa misaada wanayoitoa inawafanya kuwa karibu zaidi na jamii inayowazunguka na pia inawafanya wakubalike zaidi ndani ya jamii. Mkuu huyo wa mkoa alisema wawekezaji wanaojitenga na jamii wanakuwa hawatendi jambo jema na ndio maana wanaofanya hivyo wanakumbana na vikwazo na misukosuko toka kwa jamii inayowazunguka. Aliwataka wawekeazji waige mfano wa kiwanda cha samaki cha Vicfish hasa kazi nzuri ya kuisaidia jamii inayoizunguka, alikipongeza kiwanda hicho pia kwa kuwachimbia wananchi visima vya maji na kuongeza ajira mkoani Kagera, kiwanda kinatoa ajira ya kudumu kwa watu 400. Alikipongeza pia kiwanda hicho kutokana na kuwachimbia wananchi mabwawa ya kufugia samaki,kuanzisha mashule ya chekechea na misaada inayotolewa na kiwanda hicho kwa jamii zinazokubwa na majanga mbalimbali. Aliutaka uongozi wa manispaa ya Bukoba kuhakikisha inalinda na kuitunza bustani hiyo ili isichafuliwe na watu wasiopenda maendeleo, alisema wasipofanya hivyo watakuwa wanamvunja moyo mwekezaji alitengeneza bustani hiyo. Kwa upande wake meneja mkuu wa kiwanda cha Vicfish Nurdin Salim, katika hotuba yake alimweleza mkuu wa mkoa kuwa kiwanda hicho tawi la Bukoba lilianza mwaka 2005, alisema kiwanda hicho kimefadhili ujenzi ya mzunguko wa standi kuu ya mabasi kupitia mfuko wake unajulikana kwa jina la Bahari Bounty Trust Fund. Salim alisema mfuko huu ulianzishwa rasmi kwsa lengo la kutoa huduma za jamii, alisema mfuko huu uliundwa mahususi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kufikia lengo lake la kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Meneja huyo mkuu alimaliza kwa kuiomba manispaa ya Bukoba kupokea dhamana ya kuhudumia mzunguko huo ili waweze kuunga mkono jitihada zilizofanywa na kiwanda cha samaki cha Vicfish zenye lengo la kuupendezesha mji wa Bukoba. |
Nimependa hii. Changamoto kwa mikoa,wilaya, na maofisi, mashule.......
ReplyDelete