Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea mgonjwa toka Hospitali ya Mwananyamala tarehe 18/08/2011 akiwa mahututi na hajitambui. Inasemekana kuwa mgonjwa huyu aliokotwa na wasamaria wema barabarani akiwa amegonjwa na gari usiku wa kuamkia tarehe 18/08/2011 ambao walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala. Kwakuwa alikuwa ameumia sana Hospitali ya Mwananyalama iliamua kumleta Hospitali ya Taifa Muhimbili ili aweze kupata huduma na uchunguzi mkubwa zaidi.
Mgonjwa huyu hajulikani jina lake kwani hawezi kuongea toka alipoletwa kutokea Mwananyamala. Mgonjwa huyu alifanikiwa kuonwa na madaktari bingwa siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 na kufanyiwa uchuguzi wa vipimo mbalimbali ikiwemo X-Ray ya tumbo, kichwa, kifua na kiuno. Matokeo ya vipimo hivyo yalionekana kuwa kichwani kulikuwa na damu kidogo iliyoganda kutokana na kuvujia kwa ndani, picha za kifua na kiuno zilionyesha kuwa hakuna tatizo.
HALI YAKE:
Tangu apelekwe ICU hali yake bado ni mbaya, hajitambui. Aidha tangu tarehe 18/08/2011 hakuna ndugu au jamaa aliyejitokeza kuulizia hali ya mgonjwa huyu.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unaomba yeyote anayemfahamu mgonjwa huyu atoe taarifa kwa ndugu na jamaa zake ili waweze kuja kumtambua ndugu yao. Tunaendelea kumpa huduma zote ikiwemo chakula na dawa.
Imetolewa na:
Aminiel Aligaesha,
Afisa Uhusiano,
Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Septemba 2, 2011.
Mwanaume/mwanamke? kisio la umri? mavazi? Assume ni wewe ndiye unayepewa hii taarifa na sio kuiandaa. Ila mmefanya jambo jema kumhudumia haraka na kumpatia chakula.
ReplyDeletemichuzi samahani sikuweza kuona picha sina uhakika kama ni mimi tu au kilamtu ni hivyo hivyo.
ReplyDeletePicha hazionekani
ReplyDeletepicha hazionekani,cn u solve it pls if its technical problm.
ReplyDeleteJamani Michuzi mbona picha hazionekani?
ReplyDeletepicha tafadhali kaka michuzi!!!!
ReplyDeletembona picha hakuna ? kuna giza na alama ya kuuliza! halafu hii si mara ya kwanza kuna siku nyingine huwa baadhi ya picha huwa hazionekanagi zaidi ya giza na hii alama (?)
ReplyDeleteNaomba nichukue muda huu kuiomba meza ya hii blog kuahinisha mambo yafuatayo kuhusu huyu mgonjwa anayeelezewa hapo juu.
ReplyDelete[1].Jinsia ya mgonjwa.
[2].Kadilio la umri wa mgonjwa.[kijana,makamo,mzee. etc.
[3].Rangi ya mgonjwa.
[4]Umbile la mgonjwa ie.mfupi,mrefu,mnene,mwembamba etc.
[5]Nguo alizo kuwa amevaa mara ya kwanza kwani nadhani amebadilishiwa mavazi.
Baada ya maombi hayo,ninadhani pia kwamba,wasamalia waliomuokota eneo la tukio waliweza kupata baadhi ya mizigo au kitu chochote alichokuwa nacho huyu ndugu yetu vinavyoweza kutusaidia kumtambua.Ombi kwa blog ya michuzi,tunaomba mjitolee kwa neema ya mungu kwa kushirikiana na askali yeyote[kituo cha karibu na alipookotwa mgonjwa] na wasamalia wema waliomuokota,[nadhani waliacha mawasiliano yao Mwananyamala Hospital]ili kupata ufumbuzi wa kumtambua mgonjwa katika eneo la ajali.Unless otherwise,mpigeni picha nyingine tumtambue kwani hizi hazifunguki.
Mdau Ughaibuni.
Picha hazionekani
ReplyDeleteNA MIMI PIA SIPATI PICHA
ReplyDeleteNyie hamjagundua kitu. Hii ni enzi ya mwalimu unapigia kura kati ya Picha na kivuli. Kazi kwenu.
ReplyDeleteHizo ni picha za X-ray sio za sura ya mgonjwa. Pia hili tangazo ni kwa mtu aliyepotelewa na ndugu yake kwa muda huo wote aende hospitali akamwangalie. Tunaishi TZ utafikiri ughaibuni!!
ReplyDelete