Usiku wa kuamkia leo Moto ambao haukufahamika chanzo chake uliteketeza soko dogo lililopo maeneo ya Forest ya zamani karibu na Chuo kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria matawi ya Jijini Mbeya na kusababisha mabada kadhaa kuteketea kwa moto ambao uliwahiwa na kikosi cha zima moto cha mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mjini,Bw. Evans Balama alifika katika eneo hilo usiku huo na kusaidiana na wananchi waliokuwepo karibu na eneo la tukio na kuuzima Moto huo kabla ya kikosi cha zima moto kufika eneo la tukio.Kumekuwa na maswali mengi sana hivi sasa Jijini Mbeya ya kujiuliza,kunani katika masoko ya Mbeya mpaka kila siku yawe yanawaka moto na kwanini tahadhari hazichukuliwi mapema??
Kamera man wa Globu ya Jamii ambaye alifika eneo la tukio mapema leo asubuhi na kukuta moto umefanikiwa kuzimwa katika vibanda hivyo vilivyokuwepo sokoni hapo na haya ndio baadhi ya masalia ya mabanda hayo huku moshi ukiendelea kufuka.
Mashuhuda waliokuwepo maeneo ya jirani na soko hilo walisema Moto huo ulianza majira ya saa 9:00 kamili usiku na muda si mrefu taarifa ziliwafikia kikosi cha Zimamoto na wao walifika eneo la tukio dakika 10 baadae na kufanikiwa kuuzima moto huo bila hata ya maigizo yao ya kila siku ya kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji au kuharibika kwa gari wakati wakiwa kwenye tukio.Picha na Latest News TZ
Hapa sio bure kKna mchoma moto (arsonist) kazini. Jee anafanya hivyo kwa maslahi ya nani, yake au katumwa?
ReplyDeleteWengine hupenda tu kuona watu wanavyohangaika pale vibanda vinavyoungua. Dunia ina mambo.