Jumuia ya waumini Watanzania wa kiadventsta wasabato waishio Houston Texas wanapenda kutoa Rambi Rambi zao kwa tukio kubwa la kutisha lililowakumba ndugu zeta wa visiwa vya Pemba na Zanzibar, ni janga la kutisha sana. 

Tunapenda kutoa pia shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya maajabu ya kuokolewa kwa Idadi kubwa sana ya abiria jambo ambalo ni la kushangaza, ukilinganisha na tukio la Mv bukoba ambapo walikuwa wengi kuliko walio okolewa. 

Tunawapongeza makundi yote ya watu waliojitokeza na kujitolea kuokoa uhai wa Watanzania wenzao Mwenyezi Mungu atawabariki na kuwaongezea rehema zake kwa kujitolea mali na uhai kuokoa uhai wa wengine.

Kadhalika tunawapa pole wato waliofia na jamaa zao Mungu awatie faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mkubwa. Iadha tunawaombe walio jeruhiwa Mwenyezi apate kuwaponya na kuri kwenye shughuri zao za kujenga taifa letu.

ASante
Mchungaji P MSwanyama
Kwa niamba ya Wasabato- Houston, TX

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamni hali ndiyo hii hapa nyumbani kwa ujumla. Napenda kuchukuwa fursa hii kuwapongeza wasabato wa Houston, TX kwa kujali na kutuma salamu za rambi rambi hapa home. Kweli inasikitisha sana sisi tulioona picha mbali mbali inauma sana kuona UZEMBE uliofanyika mpaka kusababisha ajali kama hii. Nawatakia mafanikio na jamani nasikia huko AMRI YA JUMAPILI YA TAIFA INANUKIA? Nimepata taarifa hizi kutoka kwa msabato mmoja kutoka huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...