Mwenyekiti wa Rotary Club Tanzania,Harish Bhatt akimpngeza Mtoto Tamara Jo ambaye ni mmoja wa watu walionyesha mchango mkubwa kwa jamii na kuwasaidia baadhi ya watu kufanikiwa katika maisha yao.kulia ni Mjumbe wa Rotary Club Tanzania,Maninder Lamba.
 Mkurugenzi wa Miradi wa Rotary Club Tanzania,Zainul Dossa (kulia) akikabidhi tuzo pamoja na cheti kwa Ndg. Paul Luvinga ambaye amejitolea sehemu ya Nyumba yake na kuifanya ni maktaba ya vitabu vya kusoma watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wanaosoma katika ngazi mbali mbali za elimu hapa nchini.
 Mama Sharmila Bhatt wa Rotary Club Tanzania akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo kwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii.
 Baadhi ya watu waliotunukiwa tuzo hizo wakifuatilia kwa makini hafla hiyo.
Wadau wa Rotary Club Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mdau kutoka Marangu KomelaSeptember 20, 2011

    Tunakupongeza shemeji Luvinga for what you have done. Tunahitaji watu kama nyinyi ili tuweze kuendelea

    ReplyDelete
  2. Hongera sana! Mungu awabariki wote. Kila mtu akijitolea naamini kwamba tutaweza kupunguza umasikini. Si kila kitu kutegemea serekali. Tukiacha kuendekeza michango kuenda kwenya ma 'hepi besidei' na sherehe mbalimbali zisizokuwa na umuhimu, na badala yake tuchangie kujenga shule, kununua vitabu, madawati, kulipia mtoto wa ndugu aende shule, au hata kujumuika na wenzetu kusafisha mazingira yetu sisi wenyewe kweli itakuwa vibaya? Mbona ughaibuni kila kukicha watoto wadogo kama huyo hapo juu wanajitolea kuuza juisi (lemonade stand) ili kuweza kusaidia wengine. Kuna kuwaga na mbio kila baada ya miezi kadhaa na watu hushiriki ili kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa kama saratani, UKIMWI etc. au hata kusaidia watu masikini. Yote haya yanawezekana hapa nyumbani, sema tu watu hatuna mioyo ya kujitolea kusaidia jamii, lakini namba moja kwenye kurusha roho na kupokea misaada. Mwaka 2011 huu, watu wameshaanza kuchoka kila kukicha mabilioni na mabilioni yanamwagwa kwenye bara letu lakini wapi! Umasikini bado upo. Wenzetu Somalia wanakufa njaa huku dunia inaangalia. Watanzania wenzangu, inabidi tusimame kwa miguu yetu miwili ili tuweze kusonga mbele tusije achwa mbali. Tuache kutegemea wengine waje kutuokoa, tujiokoe wenyewe.

    Sorry for the long comments! I am very passionate about the idea of self determination and self reliance. Wachina hawakufika walikofika kwa kuwa omba omba. Tufanye kazi kwa nguvu zote, tujue haki zetu, tusiendekeze uzembe na starehe. Huu ni wakati wa kuchapa kazi na kuwa wakali hasa kwa viongozi wetu. At least for the sake of future generations.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...