![]() |
MAREHEMU THERESIA VERONICA RWEYEMAMUKUZALIWA 23.04.1973 KUFA 03.09.2011 |
Shukurani za pekee ziwaendee Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Lugalo, watumishi wa Mungu wa kanisa la Breakthrough - Boko chini ya uongozi wa Mchungaji Gosbert Semtomvu na kanisa la Living Water (Makuti) Kawe chini ya uongozi wa Mtume Onesmo Ndegi.
Pamoja na majirani wote, Ndugu wote, jamaa na marafiki wa familia.
Kwa kila aliyejitoa kwa namna moja ama nyingine Mungu atamlipa kwa majira sahihi, maana ulichokifanya kwetu ni kupanda mbegu na utavuna kwa kipimo cha kujazwa na kusukwa sukwa.
Tunamshukuru Mungu kwa kutuponya kidonda, maana hatuna maumivu ndani ya mioyo yetu lakini kovu haliwezi kufutika kamwe.
Daima utakumbukwa na Baba na mama yako, watoto wako Irene na Billy, kaka zako Richard, Rutakinikwa, Ndyamkama, na Rutahiwa, dada zako Felista, Anita na Devota bila kumshahau Bibi yako Theresia Rwakyendera.
Biblia inasema katika kitabu cha Ufunuo 14:13 "Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa....." japo kimwili ni mfu lakini tunaamini nafsi yako hii hai ikimtukuza na kumshangilia Bwana milele. Amina
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...