Ankal (kulia) akimkabidhi Jezi  Mpya  DJ Luke Joe  kwa ajili ya  mtanange wa Yanga na Simba za ughaibuni utakaochezwa Sept 24,2011 HUKO Manassas,Virginia,  kugombea Uhuru Cup, ikiwa ni mojawapo ya shamrashamra za kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru. Jezi  hizo ambazo ni pamoja na bukta na soksi, zimetolewa maalum kwa mpambano huo na VODACOM TANZANIA ambao ndio wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania.

TFF ya ughaibuni inatoa shukrani za dhati kwa VODACOM TANZANIA kwa kuthamini michezo hata kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi maarufu sana kama Diaspora.

Tunasema asante sana VODACOM TANZANIA na hongereni mno kwa kufikisha wateja milioni 10. Makabidhiano hayo ya jezi yalifanyika leo kitongoji cha Manhattan jijini New York,Nchini Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hivi tanzania huwa kuna simba na yanga tu? manake kila siku ni wao tu ndiyo vinara wa kupendelewa, sio fresh wala nini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...