Meneja Masoko wa Kampuni ya kuuza Magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kutangaza gari atakalokabidhiwa Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011,iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu kampuni hiyo yaliyopo Barabara ya Nyerere Rd,jijini Dar.katikati ni Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania, George Rwehumbiza pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors,Alfred Minja (kushoto) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza (katikati) wakifunua gari aina ya JEEP PATRIOT lenye thamani ya shilingi milioni 72 ambalo litakabidhiwa kwa Mrembo atakaenyakua taji la Vodacom Miss Tanzania 2011.kulia ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuuza magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (katikati) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za gari lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya atakayokabidhiwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Warembo wakilifurahia gari hilo huku wengine wakilikagua.
Yule aliyegundua madini ya TANZANITE sio nae angepewa zawadi kama hiyo jamani maana kaliingizia taifa kodi nyingi kuliko hawa mamiss!!!!!!!!
ReplyDeleteKaka wee acha tuu,watu hata hawafkirii!
ReplyDeletehizi zawadi jamani wawe wanafikiria kabla ya kuzitoa, kwa mtazamo wangu hii gari huyo miss atakae shinda sidhan kama ataweza kuimudu nikimaanisha mfano ikiharibika na mambo km hayo..
ReplyDeleteI second you ..zawadi wangekua wanatia kufuata na mmazingira na uchumi wetu. Hiyo hela wangempa ajkajiendeleze na elimu ya juu zaidi au hata kuanzisha biashara. Hiyo ni kuongezeana umasikini
ReplyDeletehaya tena naona wadau wa Muhimbili Primary School mko juu. George na Alfred. Mwalimu Ndosi atakuwa proud kuona vijana wake katika globu ya jamii
ReplyDeleteHaya sasa mabinti wa kibongo changamsheni nanihii zenu hizo, Jeep ndo hilo hapo sasa (watu wengine mind on the gutter hiyo nanihii inaweza kudhaniwa 'naniliu', kumbe ni kuchangamsha 'bongo' tu)!
ReplyDeleteLakini mnajua lina cc ngapi hiko limnyama la Jeep? Manake mitego mingine (strings), utarudi mwenyewe kufata hela ya wese, lol!