Meneja Masoko wa Kampuni ya kuuza Magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kutangaza gari atakalokabidhiwa Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011,iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu kampuni hiyo yaliyopo Barabara ya Nyerere Rd,jijini Dar.katikati ni Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania, George Rwehumbiza pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors,Alfred Minja (kushoto) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza (katikati) wakifunua gari aina ya JEEP PATRIOT lenye thamani ya shilingi milioni 72 ambalo litakabidhiwa kwa Mrembo atakaenyakua taji la Vodacom Miss Tanzania 2011.kulia ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuuza magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (katikati) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za gari lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya atakayokabidhiwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Warembo wakilifurahia gari hilo huku wengine wakilikagua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yule aliyegundua madini ya TANZANITE sio nae angepewa zawadi kama hiyo jamani maana kaliingizia taifa kodi nyingi kuliko hawa mamiss!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kaka wee acha tuu,watu hata hawafkirii!

    ReplyDelete
  3. hizi zawadi jamani wawe wanafikiria kabla ya kuzitoa, kwa mtazamo wangu hii gari huyo miss atakae shinda sidhan kama ataweza kuimudu nikimaanisha mfano ikiharibika na mambo km hayo..

    ReplyDelete
  4. I second you ..zawadi wangekua wanatia kufuata na mmazingira na uchumi wetu. Hiyo hela wangempa ajkajiendeleze na elimu ya juu zaidi au hata kuanzisha biashara. Hiyo ni kuongezeana umasikini

    ReplyDelete
  5. haya tena naona wadau wa Muhimbili Primary School mko juu. George na Alfred. Mwalimu Ndosi atakuwa proud kuona vijana wake katika globu ya jamii

    ReplyDelete
  6. Haya sasa mabinti wa kibongo changamsheni nanihii zenu hizo, Jeep ndo hilo hapo sasa (watu wengine mind on the gutter hiyo nanihii inaweza kudhaniwa 'naniliu', kumbe ni kuchangamsha 'bongo' tu)!

    Lakini mnajua lina cc ngapi hiko limnyama la Jeep? Manake mitego mingine (strings), utarudi mwenyewe kufata hela ya wese, lol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...