Waziri wa Tamisemi , George Mkuchika ( aliyesimama) akisoma sehemu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya nne inayoelezea madaraka ya Umma Serikali za mitaa na kazi zake, mbele ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ( hawapo pichani) mjini Kilosa wakati alipozungumza nao na kusisitiza namna ya kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Serikali na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bandera na kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Dendego .
Mkuu mpya wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( aliyesimama) akionesha Ilani ya Uchaguzi wa Mwaka 2010- 2015 ya CCM iliyoainisha masuala ya utekelezaji wa shunghuli mbalimbali kwa wananchi wa Tanzania wakiwemo wa Mkoa wa Morogoro na Kilosa, wakati akizungumza na Madiwani , watendaji wa Halmashauri ya Kilosa pamona na wananchi (wapili kutoka kushoto) ni Waziri wa Tamisemi , George Mkuchika aliyefanya ziara Wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...