Muwezeshaji wa Warsha ya kuwapatia wadau wa Utamaduni Nchini Uwezo wa kulinda Urithi wa Utamaduni Usioshikika toka UNESCO Bw Silverse Anami akiwapiga msasa wadau wa Utamaduni Nchini.
  washiriki wa Warsha inayoendeshwa na UNESCO ya kuwapatia wadau wa Utamaduni Nchini Uwezo wa kulinda Urithi wa Utamaduni Usioshikika
Wakwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni Nchini Bi Angelina Ngowi wengine ni wajumbe toka sehemu mbali mbali Tanzania.


Na Sixmund J. Begashe

Maafisa Utamaduni nchini wametakiwa kuhakikisha wanazitambua na kuainisha Urithi wa Utamaduni Usioshikika ambao uliopo na uliyo mbioni kutoweka ilimikakati iliyopo yakuilinda iweze kutekelezeka. 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo Utamaduni Nchini Bi Angelina  Ngowi katika warsha ya kuwapatia uwezo wadau wa Utamaduni nchini wa kuutambua na Kuulinda Uridhi wa Utamaduni usioshikika.

Bi Ngowi aliendelea kusema kuwa Tanzania mwaka huu imeridhia Utekelezaji wa mkataba wa UNESCO wa kulinda na kuhifadhi Urithi wa Utamaduni Usioshikika  wa mwaka 2003. Hivyo ni imani yake kuwa kwakupitia Maafisa Utamaduni ambao ndio wanaoishi karibu na jamii zetu watashirikiana na jamii hizo ili kutekeleza makubaliano yaliyo fikiwa kati ya Tanzania na UNESCO.

Bi Ngowi alizitaja faida ambazo Tanzania itazipata baada ya kuridhia Mkataba wa UNESCO ni pamoja na kuwa na Nguvu ya pamoja ya kuulinda Utamaduni wetu kama watanzania, kupunguza adhari za Utandawazi na hata kupata misaada ya haraka kutoka UNESCO itakayo saidia kuulinda Urithi usioshikika ambao hivi sasa upo hatarini kutoweka.

Nae Mchunguzi wa Lugha ya Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi Gertrude Joseph ambae ni mshiriki wa washa hiyo amesema kuwa warsha hiyo  imewapa uelewa zaidi wa namna ya kuulinda Urithi wa Utamaduni usio shikika na kuona umuhimu wa kuishirikisha raslimali Utamaduni katika kila mpango mkakati wa maendeleo ya nchi ili kuleta ufanisi katika malengo ya Kitaifa.

Nao wawezeshati wa washa hiyo kutoka UNESCO Bw, Silverse Anami na Julius Mwahunga wameipongeza Tanzania kwa kuwa moja kati ya nchi 26 za Afrika zilizo chukuwa uamuzi mzuri wa kuridhia mkataba huo wa Umoja wa Mataifa kwani utasaidia kupambana na mwingiliano wa tamaduni za nje ambazo zinahatarisha uhai wa Utamaduni wa Mtanzania, hivyo wamezitaka nchi za Afrika zilizobaki kuchukuwa uamuzi kama ulio chukuliwa na Tanzania.

Warsha hii ya siku tano ya uwezeshaji wa Uwezo wa Utekeleza wa Maafikiano ya 2003 wa UNESCO unaohusu kulinda Urithi wa Utamaduni usioshikika, imeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na UNESCO imewashirikisha Maafisa Utamaduni kutoka kanda zote sita nchini, Wizara ya Elimu, Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara Habari, Utamani Michezo na Utalii Zanzibar, Mfuko wa Utamaduni,Taasisi za Sanaa za Binafsi, Baraza la sanaa Tanzania(BASATA) na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) inafanyika katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...