Na Bebi Kapenya - MAELEZO,Dar es salaam

Waziri wa Afya na Ustwai wa Jamii Dkt Hadji Hussein Mponda ametoa wito kwa Taasisi zote za umma za wafanyabiashara binafsi kuhakikisha kuwa zinatumia maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) ili kuisaidia kupunguza gharama za kupeleka sampuli katika maabara nyingine nje ya nchi ili kuhakiki ubora na usalama wa dawa.

Dkt. Hadji Hussein Mponda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kwa umma juu ya hatua ya maabara ya TFDA kupata kuimarika na kuwa bora hali iliyoiwezesha kutambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa Sampuni mbalimbali za dawa na chakula kutoka ndani na nje ya Tanzania.

" Kwa kuwa maabara hii sasa inatambulika kimataifa , napenda kutoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali na watu binafsi kutumia kwa ajili kupima ubora na usalama wa sampuni za dawa kabla ya kuziuza katika jamii" alisisitiza Waziri huyo.

Alisema kuwa endapo wadau mbalimbali wataitumia vizuri maaabara hiyo sio tu wataepuka kuuza bidhaa bandia bali pia wataokoa maisha ya wanancha kwa kudhibiti kuwepo kwa dawa na chakula kisichokuwa na ubora na usalama kwa ajili ya matumizi.

Dkt . Mponda alisema kuwa dawa bandi na hata chakula ambacho sio salama kinaweza kusababisha kuzorota kwa uchumi kwa sababu wananchi wakitumia wanaweza kupata madhara ambayo yanaweza kuwasababisha kushindwa kuzalisha kwa wingi.

Alisema kuwa ili kuepuka kusambaa kwa dawa bandi ni vema wazalishaji kuhakiki bidhaa zao kabla ya kuzisambaza kwa jamii kwa ajili ya matumizi na kuongeza kuwa yoyote anayesambza dawa kabla ya kuhakikiwa ni kosa.

Aidha Dkt. Mponda aliongeza kuwa Serikali imeshaanza kufuatilia Duka zote za dawa ili kuhakiki kama wauzaji wanazosifa na taalum inayotakiwa kwa ajili ya kuuuza dawa kwa wananchi.

Maabara ya uchunguzi wa dawa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilifanikiwa kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) tangu Januari 18 mwaka huu na hivyo kupata fursa kutumia maabara hiyo katika kuchunguza sampuni mbalimbali ambapo majibu yake yatatambulika na kukubalika kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...