Jibu la tatizo na sababu iliyopelekea kuzama kwa M.V Spice Islanders wiki mbili zilizopita litapatikana baada ya kukamilika  kwa uchunguzi unaofanywa naTume ya Watu kumi iliyoundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduai Dr. Ali Mohd Sheni kufanya uchunguzi huo. 

Akizungumza na Familia za wafiwa wa ajali ya Meli ya M.V Spice Islanders katika Majimbo ya Ole,Kojani na Gando Wilaya ya Wete Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Tume hiyo itaweka wazi Ripoti itakayohusika na tatizo hilo.                                              

Balozi Seif  amesema ripoti hiyo itatoa muongozo wa namna ya Taifa na Umma wote utakavyoweza kukabiliana na maafa yatakayotokea siku nyengine zijazo.  

 Alisisitiza kwamba Serikali  itajitahidi kuona  vyombo vya usafiri vinakuwa imara na kamwe haitasita kuzuia chombo chochote kibovu kwa lengo la kulinda usalama wa abiria na mali zao.                     

Balozi Seif ametahadharisha kwamba  taratibu lazima zifuatwe na hili litafanikiwa iwapo ushirikiano wa pamoja utapatikana kati ya Wananchi,Serikali pamoja na Taasisi zinazosimamia masuala hayo.    

’’ Tunachotaka sasa ni kuhakikisha kwamba abiria wanasafiri kwa njia ya usalama, hatutaki melki zijiendee bila ya ukaguzi ’’. Alisema Balozi Seif.                                                                                       

Amesema ni vyema Wananchi wakaongeza mashirikiano yao  na serikali ili kuona  Sekta ya usafiri inaendelea kutoa huduma kwa uhakika na kuaminika.       
                                                                      
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliendelea kuwaomba wafiwa kuwa na moyo wa subra kwani subra ni  nusu ya amani.    
                                                                                                               
Balozi Seif Ali Iddi amekamilisha ziara yake ya kuzifariji familia za wananchi waliofariki kwa ajali ya Meli ya M.V Spice katika Majimbo ya Ole, Kojani na Gando yaliyomo ndani ya Wilaya ya Wete Kisiwania Pemba.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
27/9/2011. 
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZAZNZIBAR MHE.BALOZI SEIF ALI IDDI AKISALIMIANA NA WAFIWA WA MAJIMBO YA WILAYA YA WETE KISIWANI PEMBA ALIPOFANYA ZIARA YA KUWAPA POLE ALIPOKUTANA NAO KATIKA MAJENGO YA SKULI YA GANDO LEO.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...