Ajali ya basi la Kampuni ya Southern Coach katika kijiji cha Miteja, Kilwa, Mkoani Lindi, iliyotokea leo majira ya saa 8 mchana. Kwa mujibu wa mashuhuda, hakuna aliyefariki japo kulikuwa na majeruhi walioumia vibaya na kukimbizwa hospitali. Chanzo cha ajali bado hakijajulikana
Sehemu ya nyuma ya basi lililopata ajali leo
Wanakijiji wakiangalia kama kuna abiria aliyenaswa ndani ya .
Picha zimeletwa na mdau kwa kutumia simu yake ya iPhone 4

Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila (kulia) akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Noordin Babu (hayupo pichani) ahakikishe majeruhi,Abiria wengine wawe wamesaidiwa usafiri wa haraka na kuamuru gari zilizo katika msafara wake ikiwemo yake kubeba majeruhi hao. Shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Saidi Meck Sadiki.

Abiria waliokuwa wakisafiri toka Dar es salaam kwenda Mtwara na Basi la Ng’itu lenye namba za Usajili T 804 BAF wamenusurika kifo baada basi hilo kupinduka katika kijiji cha Sinza –Miteja wilayani Kilwa ,Mkoani Lindi Katika ajili hiyo zaidi ya abiria 35 waliumia vibaya na kukimbizwa katika hospital zilizo jirani na ajali hiyo.

Ajali hiyo iliyoshuhudiwa na Wakuu wa Mikoa ya Dar es salaam na Lindi, Mh Saidi Meck Sadiki na Mh Ludovick Mwananzila walipokuwa katika Makabidhiano ya Mkoa huo kufuatia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufanya
mabadiliko ya vituo kati ya Aliekuwa mkuu wa mkoa wa Lindi,Ally Nassor Rufunga kubadilishana vituo na aliekuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ludovick Mwananzila kupangiwa Lindi

Chanzo cha ajali hiyo kwa Mujibu ya Abiria walioongea na Mdau wa blog hii wameeleza ni mwendo kasi ulichangiwa na kufukuzana kwa mabasi yaliyoongozana kuelekea Tunduru,Masasi,Nachingwea na Newala

Wakati huo huo watu wawili wamekufa papo hapo mkoani Mbeya baada ya gari ya wagonjwa waliokuwa wakisafiriki kupinduka Taarifa hii imeletwa na mdau Abdulaziz video Rec aliyeshuhudia ajali
hiyo aliyefika dakika 5 baada ya ajali kutokea


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...