Na Francis Godwin
CHUO kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira Iringa kimepanua wigo wa utoaji wa kozi mbali mbali kama njia ya kuwavutia watu wengi zaidi kuendelea kupata elimu ya juu hapa nchini.

Mkuu wa wa chuo cha Tumaini Makumira Iringa Profesa Nicholaus Bangu aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na kwa niaba yake na makamu mkuu wa chuo cha Tumaini Makumira Prof.Joseph Parsalaw wakati wa sherehe za mahafali ya 14 ya chuo hicho .

Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa kimepanua wigo wa utoaji wa kozi mpya zaidi ya tano ikiwemo ya Shahada ya uzamili katika sheria,Shahada ya uzamili katika maendeleo ya jamii na usimamizi wa miradi, Shahada ya uzamili wa Misioni na maendeleo ya jamii na shahada ya uzamili katika Saikolojia ya ushauri Nasaha.

Kozi nyingine ni Shahada ya kwanza ya elimu yenye michepua ya masomo ya Historia, Kiswahili, Jiografia na kiingereza pamoja na kuanzisha masomo ya jioni ya shahada, stashahada na astashahada kwa vituo vya Iringa na Mbeya.

Akiwahutubia  wahitimu 1062 waliohitimu chuoni hapo katika Mahafali ya 14 alisema na idadi yao katika mabano alisema kuwa kati ya wahitimu hao ni pamoja na wahitimu 74 waliotunukiwa shahada ya uzamili katika utawala wa biashara,( 7 )Stashahada ya Uzamili ya Uongozi,( 3 )stashahada ya uzamili ya elimu (Ufundishaji) na 18 ni wa stashahada ya uzamili ya elimu (utawala).

Aliwataja wahitimu wengine na idadi yao kwenye mabano kuwa ni wa shahada ya uandishi habari (35), shahada ya theolojia-Divinity (9), Shahada ya Sheria (172), shahada ya utawala wa biashara (110), shahada ya elimu katika hisabati (82), shahada ya ushauri nasihi (58), Shahada ya Maendeleo ya Jamii (205), shahada ya sayansi ya Technolojia ya habari-IT (30) na Shahada ya Athropolojia ya Utamaduni na Utalii (139).Wahitimu wengine waliotunukiwa ni pamoja na wale wa stashahada ya theolojia (14), cheti cha utawala wa biashara (88), cheti cha theolojia (12) na cheti cha sheria (6).

Pia alitaja baadhi ya shughuli ambazo zimekuwa zikiendelea kufanyika chuoni hapo kuwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa jingo la mafunzo ya sayansi katika fani ya fizikia ,kemina ,Biolojia na kilimo .

Aidha alisema kuwa chuo hicho kimeendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora katika vituo 43 katika maeneo ya vijijini kwenye wilya ya Kilolo,Iringa na Njombe kupitia taasisi ya maendeleo ya kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hongereni saaaana wahitimu endapo tu mlitumia oblangata zenu wenyewe bila kudesa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...