Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova huku Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba akiangalia.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.
 Bondia Francis Miyeyusho ampatia konde kali sana mpinzani wake,Mbwana Matumla wakati wa mchezo wao uliomalizika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall.Francis Miyeyusho kanyakua ubingwa katika mchezo huo kwa kushinda Mbwana Matumla kwa point.
 Hapa ilikuwa ni piga nikupige.
 chukua hiyoooo.....,holaaaaa.. kiukweli mpambano huu ulikuwa ni mkali sana na wakusisimua.
Bondia Francis Miyeyusho akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuunyakua ubingwa wa UBO usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huu mpambano naona ulikuwa mzuri na wachezaji wamecheza kiutu uzima hakuna kukumbatiana ngumi ziko wazi ,safi sana.

    ReplyDelete
  2. hongera saana miyeyusho nilitaka sana ushinde, na mwili wako uko shupavu tofauti na huyo uliye mchapa endelea kujifua wakija tu tandika!

    ReplyDelete
  3. kwenye tenis tunasema bai bai kwa williams family, kwenye ngumi za tanzania matumla family bai bai...

    ReplyDelete
  4. Miyeyusho safi sana. kweli ilikuwa wiki njema kwa rangi ya njano! ongeza juhudi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...