Hayati Maulid Hamad Maulid
Chama cha Wananchi CUF kimepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mwandishi Mwandamizi wa habari nchini Maulid Hamad Maulid ambacho kimetokea leo Mjini Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kinaamini kuwa kifo ni haki ya kila kiumbe hai duniani na kwamba hakuna atakayeweza kukiepuka pale muda ukifika hivyo ndivyo ilivyojiri kwa ndugu yetu Maulid Hamad Maulid na kwamba hiyo ni kudra ya Mwenyezi Mungu.

Nidhahiri kwamba taarifa hizi za kifo zimewagusa wengi kuanzia familia yake, taasisi alizoweza kuzitumikia zikiwemo vyombo mbali mbali vya habari, michezo, vyama, jamii na umma kwa ujumla.

Marehemu Maulid alikuwa sehemu muhimu ya jamii katika harakati za habari, Mwandishi hodari na Mahiri, mwenye kujali uzalendo, msatahamilivu na aliyeweza kushikamana bega kwa bega na wanahabari wengine pamoja na wananchi katika kuhamasisha maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Chama cha Wananchi CUF kinaungana na taasisi zote zilizoguswa na kifo cha Maulid pamoja na wananchi katika kuyakumbuka yale mema ya mjenzi huyo mashuhuri hasa wakati huu wa msiba.

Chama cha Wananchi CUF kinatoa mkono wa pole kwa familia ndugu jamaa, marafiki na taasisi pamoja na wananchi wote kutokana na kifo cha mwanahabari huyo mwandamizi.

Aidha Chama cha Wananchi CUF kinamuombea marehemu Maulid Hamad Maulid makaazi mema huko Akhera, Aamin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mzee Maulidi leo umetuacha hapa duniani na sisi tuko nyuma yako pindi siku yetu itakapofika.

    Umelitumikia taifa vyema kwa kutupasha habari mbali mbali kama wajibu wako kikazi.

    Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi AMIN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...