Dkt. David Marcel Mosha (pichani), Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi za Wakurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya Inter-Consult pamoja Akiba Commercial Bank, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo kiasi cha saa Tano asubuhi katika mji wa Kibuku, kilometa kadhaa toka Korogwe, mkoani Tanga.


Mmoja wa Wakurugenzi wa Inter-Consult Dkt. Strato P.  Mosha  kathibitisha habari hizo punde, na kusema kuwa mareheu alikuwa akisafiri yeye na dereva wake kutoka Dar es salaam kuelekea Moshi, kabla gari lake aina ya Toyota Double Cabin halijaacha njia na kupinduka kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.


Dkt Strato Mosha amesema mipango ya mazishi itafanywa baada ya mwili wa marehemu ambao uko katika chumba cha maiti cha hospitali ya Wilaya ya Korogwe utapoletwa nyumbani kwake Mbezi Chini, karibu na mafleti ya BOT, na kwamba tayari timu imeshaondoka kwenda Korogwe.


Amesema dereva wa marehemu yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi na hali yake inaelezwa kuwa ina 'stabilise' .


Kwa mujibu wa Dkt. Strato Mosha, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kwa miaka 12 kabla ya kustaafu mwaka 1978 na kubakia Mkurugenzi. Pia ameitumikia Akiba Comercial Bank kwa miaka 10.kabla ya kustaafu mwaka jana na kubakia mjumbe wa bodi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. RIP DR Mosha. Our condolences to your family.

    ReplyDelete
  2. RAHA YA MILELE UMPE MAREHEMU DAVID EE BWANA NA NURU YA USO WAKO UMWANGAZIE NEEMA NA HURUMA ZAKO ZISIZO NA UKOMO UMJALIE APUMZIKE KWA AMANI. AMINA
    HUMPHREY T. LYIMO

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu zangu.... I was shocked to learn this sad loss.... My his soul rest in peace...amen
    From T. Mosha
    Clev. Ohio

    ReplyDelete
  4. utakumbukwa daima kwa mchango wako mkubwa kwenye engineering industry, Mungu awafariji na kuwatia nguvu familia

    ReplyDelete
  5. Dominic MoshaOctober 11, 2011

    RIP Mzee David Mosha

    Wahandisi tunajua na tunafahamu mchango wako katika sekta. Umeacha Legacy.

    Wajasiriamali wanajua mchango wako kupitia Akiba Commercial Bank, hii pia ni Legacy.

    Wanakilimo wanaufahamu pia mchango wako katika kufufua zao la katani, hii pia ni legacy.

    Sekta ya usafirishaji pia wanafahamu mchango wako mlipoamua kuiondoa KIA matatizoni. Huu ni Urithi pia.

    Mwenyezi Mungu akupokee kwenye makao yake ya Milele.

    Raha ya Milele umpe ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie apumzike kwa amani.

    Poleni sana Martin, Marcel,na familia nzima kwa ujumla wote.

    Mhandisi.

    ReplyDelete
  6. Dear Chairman, upumzike kwa amani ya bwana, Mungu ndie hupanga nani na lini amtwae, AMINA

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa......sad news, nilimjua Dr.Mosha, alikuwa mwingi wa busara jamani. RIP

    ReplyDelete
  8. RIP Dr.Mosha Inter-Consult Founder.

    ReplyDelete
  9. MUNGU amjalie raha ya milele, poleni wafiwa.

    Inter Consult itamkosa the great visionary wao ambaye aliiongoza kwa busara na mafanikio mazuri.

    Kuweka record sawa, Michuzi jina la marehemu ni David Marcel Mosha,mwaka 1978 ndio alianzisha inter consult baada ya kustaafu kama Chief Engineer East African Railways, Mkurugenzi wa inter consult ni Dr Strato P. Mosha na sio Stratto au Startto.

    ReplyDelete
  10. Martin KessyOctober 12, 2011

    Rest In Peace Uncle.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana familia ya Dr. Mosha....Mungu alilaze roho ya marehemu pema peponi Amina. Pole sana Martin mungu awape moyo wa uvumilivu kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...