
Mmoja wa Wakurugenzi wa Inter-Consult Dkt. Strato P. Mosha kathibitisha habari hizo punde, na kusema kuwa mareheu alikuwa akisafiri yeye na dereva wake kutoka Dar es salaam kuelekea Moshi, kabla gari lake aina ya Toyota Double Cabin halijaacha njia na kupinduka kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.
Dkt Strato Mosha amesema mipango ya mazishi itafanywa baada ya mwili wa marehemu ambao uko katika chumba cha maiti cha hospitali ya Wilaya ya Korogwe utapoletwa nyumbani kwake Mbezi Chini, karibu na mafleti ya BOT, na kwamba tayari timu imeshaondoka kwenda Korogwe.
Amesema dereva wa marehemu yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi na hali yake inaelezwa kuwa ina 'stabilise' .
Kwa mujibu wa Dkt. Strato Mosha, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kwa miaka 12 kabla ya kustaafu mwaka 1978 na kubakia Mkurugenzi. Pia ameitumikia Akiba Comercial Bank kwa miaka 10.kabla ya kustaafu mwaka jana na kubakia mjumbe wa bodi hiyo.
RIP DR Mosha. Our condolences to your family.
ReplyDeleteRAHA YA MILELE UMPE MAREHEMU DAVID EE BWANA NA NURU YA USO WAKO UMWANGAZIE NEEMA NA HURUMA ZAKO ZISIZO NA UKOMO UMJALIE APUMZIKE KWA AMANI. AMINA
ReplyDeleteHUMPHREY T. LYIMO
Poleni sana ndugu zangu.... I was shocked to learn this sad loss.... My his soul rest in peace...amen
ReplyDeleteFrom T. Mosha
Clev. Ohio
utakumbukwa daima kwa mchango wako mkubwa kwenye engineering industry, Mungu awafariji na kuwatia nguvu familia
ReplyDeleteRIP Mzee David Mosha
ReplyDeleteWahandisi tunajua na tunafahamu mchango wako katika sekta. Umeacha Legacy.
Wajasiriamali wanajua mchango wako kupitia Akiba Commercial Bank, hii pia ni Legacy.
Wanakilimo wanaufahamu pia mchango wako katika kufufua zao la katani, hii pia ni legacy.
Sekta ya usafirishaji pia wanafahamu mchango wako mlipoamua kuiondoa KIA matatizoni. Huu ni Urithi pia.
Mwenyezi Mungu akupokee kwenye makao yake ya Milele.
Raha ya Milele umpe ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie apumzike kwa amani.
Poleni sana Martin, Marcel,na familia nzima kwa ujumla wote.
Mhandisi.
Dear Chairman, upumzike kwa amani ya bwana, Mungu ndie hupanga nani na lini amtwae, AMINA
ReplyDeletePoleni sana wafiwa......sad news, nilimjua Dr.Mosha, alikuwa mwingi wa busara jamani. RIP
ReplyDeleteRIP Dr.Mosha Inter-Consult Founder.
ReplyDeleteMUNGU amjalie raha ya milele, poleni wafiwa.
ReplyDeleteInter Consult itamkosa the great visionary wao ambaye aliiongoza kwa busara na mafanikio mazuri.
Kuweka record sawa, Michuzi jina la marehemu ni David Marcel Mosha,mwaka 1978 ndio alianzisha inter consult baada ya kustaafu kama Chief Engineer East African Railways, Mkurugenzi wa inter consult ni Dr Strato P. Mosha na sio Stratto au Startto.
Rest In Peace Uncle.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Dr. Mosha....Mungu alilaze roho ya marehemu pema peponi Amina. Pole sana Martin mungu awape moyo wa uvumilivu kipindi hiki kigumu.
ReplyDelete