Na Ankal
Jana Jumapili Oktoba 30, 2011 historia mpya imewekwa katika Nyanja ya habari, hususan sekta ya habari kwa njia ya mtandao, pale Blogu ya 8020 Fashions inayomilikiwa na Da’Shamim Mwasha ilipofanya sherehe kubwa sana ya kutimiza miaka 5 ya uhai wake katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Jana Jumapili Oktoba 30, 2011 historia mpya imewekwa katika Nyanja ya habari, hususan sekta ya habari kwa njia ya mtandao, pale Blogu ya 8020 Fashions inayomilikiwa na Da’Shamim Mwasha ilipofanya sherehe kubwa sana ya kutimiza miaka 5 ya uhai wake katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
![]() |
Da'Shamim Mwasha a.k.a Shamim Zeze |
Historia imewekwa kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kabisa kuandaliwa sherehe iliyohudhuriwa na watu wengi (takriban 600 hivi), wengi wao wakiwa Wanawake waliojitokeza kumuunga mkono Da’Shamim kwa Blogu yake kufikisha muda huo. Na wote walifanya hivyo wakiwa wamevalia nadhifu mavazi yaliyowapendeza sana ya vitenge na khanga katika kuuenzi utamaduni wa Kitanzania.
Wengi walishangaa, na bado wanashangaa imewezekana vipi Blog tu, tena Blogu ya Mitindo, kuweza kuvuta hisia za watu kiasi kile. Fanaka ya Blogu ya 8020 Fashions sio tu imedhihirisha kwamba sekta ya habari kwa njia ya mtandao imewasili rasmi nchini Tanzania. Anayieibeza anafanya hivyo kwa bahati mbaya, aidha kwa kutojua umuhimu wake ama bado hajaamka usingizini kwamba hii ni karne ya 21 na dunia imekuwa kijiji. Maana tutake tusitake fani ya kupashana habari kwa njia ya mtandao imeshajikita katika mstari, anayechelewa kujiunga atakuja kujuta baadae.
Ankal na Blogga hodari Da' Jane John (shoto) na Da'Shamim |
Kwa niaba ya timu nzima ya Globu ya Jamii pamoja na wadau wake wote duniani kote, nachukua nafasi hii kuipongeza Blogu ya 8020 Fashions kwa kutimiza miaka 5, na pia kumpa hongera Da’Shamim kwa kuweza kuanzia chini hadi kukwea daraja na kuwa Blogga anayeongoza katika fani kwa upande wa Wanawake na hata kwa wanaume pia. Hilo halina ubishi, ushahidi ni hiyo sherehe yake iliyofana utadhani ilikuwa ni Kitchen Party ama Send off ya mtu yeyote aliye maarufu katika jamii.
Nichukue nafasi hii kwa kumsifia Da’Shamim sio tu kwa kutimiza miaka 5 ya Blogu yake, bali pia kwa kuwa karibu na jamii na Mablogga wenzie kwa muda wote huo, akiendeleza Libeneka kwa ustadi, weledi na nidhamu ya hali ya juu. Vile vile, sera yake ya kujikita kwenye sekta ya Mitindo, ambayo inahitji promosheni kubwa ili ikuwe zaidi, ni mfano wa kuigwa.
Ni mfano wa kuigwa na pia ni changamoto kwa wadau kuanzisha Blogu ama tovuti za kila fani na sekta. Tunahitaji Blogu ama tovuti nyingi zitazojikita katika fani mbalimbali, zikiwemo burudani, michezo, kilimo, elimu, afya, maendeleo ya jamii na watoto na kadhalika. Wigo ni mpana mno na unahitaji kujazwa, ikizingatiwa hivi karibuni Tanzania itakuwa imejiweka katika njia kuu ya mawasiliano duniani mara utandikaji wa Mkongo wa Taifa (Fibre Optic) unaokwenda kwa kasi nchi nzima utakapokamilika na kurahisisha utendji na kuongeza kasi na kuleta unafuu wa gharama.
![]() |
Da'Shamim na Ankal baada ya kupewa tuzo za ubora wa Blogu zao hivi karibuni |
Nasema hivyo kwa sababu watu wengi wanapenda kuanzisha Blogu, ila tu wengi wanadhani Blogu ni habari na mapicha ya matukio tu. Wanasahau kwamba asili ya Blogu ni fursa ya mtu kuweka mtandaoni mambo yake binfasi na kuwaeleza walio karibu yake nini amefanya na wapi. Dhana ya kuwa Blogu ni habari imekuja baada ya sisi Tanzania kuanza kuzijua Blogu kwa mtindo huo. Yaani wengi wetu tumezijua Blogu zenye habari na mapicha na kuwa na wazo kuwa hiyo ndio kazi yake.
Katika kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, inabidi tujifunge kibwebwe kwa kutambua kwamba habari ni nguvu na kwamba kila chombo cha habari, iwe baragumu ama gazeti, TV, redio na sasa Blogu, tovuti na kadhalika, vina nafasi kubwa katika kuchangia kasi ya maendeleo ya nchi.
Da'Shamim na Mwamvita Makamba |
Nimalizie kwa kushukuru mno makampuni mbalimbali kama vile VODACOM, TBL, SBL, NMB, NBC na kadhalika ambayo kwa kutambua umuhimu wa habari kwa njia ya mtandao, yamekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Blogga wa Tanzania kwa hali na mali, kwani udhamini wanaotoa sio tu unampa nafuu Blogga katika kutekeleza majukumu yake pia mashirika na makampuni hayo yanachangia kwa kiwango kikubwa katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika sekta ya habari.
Ombi letu ni kuwa waliokwishaanza kusaidia wanahabari wa mtandaoni waendelee kufanya hivyo, na wanaosita tunawaomba wafunguke na kutoa msaada.
Hongera Da’Shamim. Kaza buti.
Kazi ndio kwanza imeanza. Onesha njia zaidi
Libeneke Oye!
Congrats sister Shamim. Tunakutakia kila la heri.
ReplyDeleteHongera Zeze na timu yako nzima ya 8020.
ReplyDeleteMiaka 5 si mchezo, nakumbuka enzi zile 8020 ilipoanza kuchomoza kipindi kileee... kuleeee... michokeni.
KK - "Mtoto wa Mwalimu"
Tembeatz.blogspot.com
Mmmh!!!!!!!! Mtoto jicho hilo!! But you look gud. Bigup kwa kazi nzuri.
ReplyDelete