Jeshi la Polisi nchini kupitia Inspekta Generali Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambaye alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto. mtoto huyo alinusurika kuuwawa baada ya kumng'ata mtu huyo sehemu za siri...
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa kabisa.
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi
Mdau Geita
Je kuna ushahidi wowote kuwa hivi viungo vya albino vinatumika kwenye uchawi na kuleta mafanikio kwa wenye kufanya huo uchawi?
ReplyDeletehakuna haja ya kuuliza swali kama hilo kwani tumepoteza ndugu zetu wengi sana, kwa hiyo swali lako sidhani kama linahitaji jibu la ndiyo au hapana kwa sababu vyote kwa pamoja havina maana.
ReplyDeleteThe hunting of albinos for body parts - just one more kind of horrendous harm that supernaturalistic thinking, and lack of proper education can bring about. There are no harmless superstitions, because even the most inocuous enforce a world view where magic actually works, and where claims like albino body parts having magical powers are made plausible. Our beliefs inform our actions, and superstitious beliefs inform irrational behavior, that can often lead to harm for the believer, and/or others around them. There is no justification for this, I loathe these monsters that rain terror fellow Tanzanians.
ReplyDeleteMdau wa Geita unatisha! Mtoto wa miaka 14 anacharangwa kama mshikaki, halafu unalalamikia kodi dhidi ya kumtafuta mhalifu! Unafikiri hao wanaowatuma watapatikana vipi ikiwa huyo aliyetumwa hajapatikana? Saheme on you man!
ReplyDeleteKweli binadamu tunatofautiana, alieuliza swali hapo juu sijui mwenzetu kaguswa na kipi ambacho ni muhimu kwake. Mungu tusaidie!
ReplyDelete