Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' leo Jumanne tarehe 18-10-2011 inatarajia kufanya onyesho maalum kwa ajili ya kuwasikilizisha waalikwa maalum nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu yao mpya iitwayo Dunia Daraja itakayozinduliwa mwezi ujao tarehe 06-Novemba-2011.

Albamu hiyo mpya itakuwa na nyimbo sita ambazo ni 'Dunia Daraja' uliotungwa na Charlz Baba, 'Umenivika Umasikini'

uliotungwa na Lwizer Mbutu, 'Mtoto wa Mwisho' uliotungwa na Dogo Rama, 'Penzi la Shemeji' uliotungwa na Mwinjuma Muumini, 'Mapenzi Hayana Kiapo' uliotungwa na Saleh Kupaza na 'Kauli' uliotungwa na Rogart Hegga.

Waalikwa mbalimbali wamealikwa kwa ajili ya listening Party ya twanga kama wanamichzo maarufu, Wanamitindo, Wacheza filamu, Makampuni ya simu, kampuni za Bia, Mabenki mbalimbali, wadau wa sanaa na burudani, BASATA, COSOTA na WANASIASA. wengine ni waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Baada ya onyesho hilo la Listening party, Twanga Pepeta itafanya uzinduzi wa Albamu yake mpya ya 'Dunia Daraja' tarehe 06-11-2011 katika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Jijini Dar es salaam.

HASSAN REHANI.
MRATIBU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...