kaka michuzi napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe na wapiganaji wote wa glob yako!kwani mmekuwa mstari wa mbele kwa utoaji taarifa muhimu kwa jamii.

kaka baada ya hilo,tunaomba kutoa tuliyonayo moyoni!mnamo usiku wa kuamkia jumatano,kigamboni maeneo ya kibada kulitokea tukio la ujambazi,mkubwa wa kutumia silaha.

kutokana na eneo lenyewe kugubikwa na matukio ya namna hiyo kila mara,wakazi wa kibada wenye moyo wa kujitolea wameanzisha kikundi cha kujilinda na matukio kama hayo ambacho ni ulinzi shirikishi,kwa hiyo siku hiyo baada ya kikundi hicho kupata taarifa kwamba majambazi yamevamia kanisani na kujeruhi mlinzi,kumfunga kamba mchungaji na kupora vitu vya thamani vya kanisa.

kikundi kiliyazingira majambazi,na kuweza kukamata majambazi matano,kati ya hayo majambazi,matatu yalipelekwa kituo cha polisi cha mji mwema na raia waliojitolea kwani mpaka wakati huo polisi walikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliejitokeza,si wa mji mwema wala kigamboni.

baada ya kuwafikisha hao majambazi kituoni mji mwema ,askali wa zamu kituoni walikataa kuwapokea majambazi,kwa kudai kwamba hawana uwezo wa kuwaweka pale na badala yake raia wema wawapeleke kituoni kigamboni!!baada ya hao raia wema kuona hamna jinsi ikabidi safari ya kigamboni ianze,but kabla hawajafika mbali yale majambazi yaliwashinda nguvu hao raia wema na kutoroka!!!

cha pili raia wema katika tukio hilo waliyakamata magari mawili ,moja toyota gx 100 na jingine ni toyota hiace yakiwa yamesheheni mizigo ya wizi!,ambapo hilo moja gx 100 ni la polisi mwanamke wa changombe!!! 

lakini kwa hari ya polisi kigamboni ilivyo hatutashangaa kuona hata hayo magari yameachiwa huru yaendelee na kazi za kishenzi za ujambazi,kwani kama watuhumiwa wanagoma kuwapokea!!!na mambo yanaendelea kama kawaida hakuna uwajibishaji wala nini!!tukiwa kama wana kigamboni tunaomba hili mheshiwa kamanda kanda maalum,Afande KOVA ulivalie njuga.

wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu na pia majambazi wote wapatikane na mkono wa sheria uchukue mkondo wake.tunaomba kaka usituminyie utuwekee hewani hii wadau waione wachangie kwani sauti ya mnyonge ni kalamu!!

wadau wa Kigamboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Poleni sana na matatizo,na vilevile nawapongeza wananchi kwa kujitolea.Na baada ya yote hayo ningeomba siku nyingine mkiwakamata tena ningewaomba muwavunje miguu yao yote kwa sababu suala la kuchoma moto binaadamu huwa nalipinga.Na wasingetoroka kama mgewavunja miguu yao na kwa maumivu wangeyapata ingekuwa na fundisho na adhabu maana hatujui kama watakaa jela au watarudi mitaani kuendelea na ujambazi.Na hayo magari kitu mngefanya ni kutoa vitu vya wizi na kuvihifadhi halafu mngeyachoma moto na kama ni la polisi tena kivyake.

    ReplyDelete
  2. Daw ni kuwapiga moto maana hapo iko wazi kuwa jeshi la polisi linahusika.....Ndugu zetu ni wajibu wenu kuchukua sheria mkononi kama chombo husika hakiko tayari kufanya hivyo...Hawa watu wanaua na kupora mali za watu kwa kujiamini, sasa dawa mnayo wenyewe andaaeni mataili ya kutosha na magaroni ya petroli....HII RUSHWA ITATUMALIZA...JK UMESIKIA?

    ReplyDelete
  3. WNANAWAFAHAMU NDO MAANA WALIGOMA KUWAPOKEA. NINACHOJUA MIMI WALITAKIWA WAWAPOKEE HATA INGEKUA KUWAPELEKA HICHO KITUO KINGINE WANGEKUA UNDER ESCORT YA POLICE, INCH IMEKWISHA KILA MTU ANAWAZA TUMBO LAKE HAKUNA MWENYE UCHUNGU NAYO YANAYOTEKEA SASA NI AIBU

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa kuanzisha kikundi cha ulinzi shirikishi. Nami nimesikitishwa na taarifa hii. Poleni kwa yote yaliyowasibu. Naomba tuwasiliane ili niweze kufuatilia tukio hili. Nitumie namba yako kupitia Kigamboniyetu@gmail.com nitakupigia.
    Ahsante
    Dr Faustine Ndugulile
    Mbunge Kigamboni

    ReplyDelete
  5. N ikweli Polisi wa Kigamboni wanazembea sana wakiiitwa kuna tukio kazi kula rushwa tuu kuna matukio kibao hawajali kabisa.

    ReplyDelete
  6. Wadau wa Kigamboni kwanza ninawapa hongera sana kwa kazi nzuri uliofikiria kuifanya na kufanikiwa kuwakamata wahalifu!kwakweli inasikitisha kwa jeshi lapolisi kuwafanyia haya sisi wadau wa jamii pia tunafikiria mpigane mpaka ocd aachie ngazi kwakweli hafai kwanza mnahitaji pongezi sbb mmewasaidia kazi na pia mmerizki maisha yenu na hili swala pia kama muheshimiwa Raisi ama mkuu wa polisi akiliachia lipite basi Tanzania sio nchi yakuitwa nchi!Inatisha kama criminal wanapatika polisi hakuna?kwakweli Said mwema unakabiliwa na kashfa nyingi bora uachie ngazi na polisi wengi ndio majambazi sijui hii nchi inakwenda wapi!Ndugu zangu sasa hivi mkikamata mko na haki yakutia moto ndio ushauri wangu mkubwa ndio polisi watakuja wenyewe kuchukuwa mzoga!

    ReplyDelete
  7. Poleni sana kwa kazi ngumu mlioifanya,msichoke na msikate tamaa,hilo suala lipelekeni mbele na muandike malalamiko yenu ili mupeleke kwa wahusika wa ngazi za juu,hata kama kwa waziri wa mambo ya ndani,lazima tatizo lishughulikiwe msinyamaze kimya,maana mkinyamaza na rushwa itazidi kunuka bongo,haki haitotendeka!Muwe na umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

    ReplyDelete
  8. polisi wametupa utu na ubinaadam mbele ya pesa,mwaka 2005 majambazi waliniulia mume wangu mpendwa na kuniacha mimi na watoto wangu wakiwa,yaani nina maaumivu makali sana hadi leo kwa kuondokewa na mume wangu,majonzi na maumivu bado hayajaniisha,halafu nilivyokuwa naenda kituo cha oysterbay kuulizia kila mara kuhusu tukio hilo kama wamewakamata majambazi hayo,Eti nikawa naambiwa na mkuu wa upelelezi kuwa kuna watu wamekamatwa lakini upelelezi bado unaendelea!Kama haijapita rushwa ni nini hapo?Upelelezi gani huo usioisha na sasa ni miaka sita imeshapita?Mie sina uwezo wowote ila iliyobaki namwachia Mnyeezi Mungu.

    ReplyDelete
  9. Najuwa sever umeiminya coment yangu lakini huyu mbunge anataka watu wamfate badala yeye atafute watu wake waliompa kura ili awape hamasa na kupanga mikakati yakuondoa polisi wala rushwa na kuleta vituo vya polisi anataka yeye afatwe kwa mkewe mimi naona yeye yuko pamoja na hao polisi wazembe!

    ReplyDelete
  10. Hapo nyie mkiwakamata wavunjeni mishipa ya visigino vyao wala msiwapige wala kuwachoma moto hiyo inatosha hivyo tutawatambua kila kona watakoweza kupita akirudi mkono wa kulia akirudia tena wa kushoto tena mkiukata chimbeni shimo muufukie msisubiri polisi kwani mtakuwa mmewapunguzia kazi kwani mnamkamata jambazi siku ya pili unamwona tena mtaani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...