Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ufunguzi wa mashindano ya Mitumbwi kwa mwaka 2011 jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Meneja wa Bia ya Balimi,Edith Bebwa.
Meneja wa Bia ya Balimi,Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2011. 

Mashindano hayo ya kupiga kasia, yanayo dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager”  yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe.

 Mashindano haya yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka. 

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka sita sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, "kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika" alisema Bebwa. 

Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa.  

Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza tarehe 18 Desemba. 

Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Mwanza tarehe 23 Oktoba, Kigoma na Kagera tarehe 5 Novemba, Mara na Ukerewe tarehe 19 Novemba. 

Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu tatu za wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu zaidi katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza. 

Zaidi wataochukuwa ubingwa mwaka huu upande wa wanaume na wanawake watapata  fursa ya moja kwa moja ya kuingia finali za mwaka ujao ili kutetea ubingwa wao.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Masoko wa Tbl Bwana Fimbo Butallah alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo:


Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu
Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake
Mshindi wa kwanza                 800,000                  600,000               2,600,000                  2,200,000
Mshindi wa Pili                 600,000                  500,000               2,200,000                  1,600,000
Mshindi wa Tatu                 400,000                  300,000               1,600,000                     850,000
Mashindi wa Nne                 350,000                  250,000                   850,000                     600,000
5 hadi 10 - Kila timu                 200,000                  150,000
                  400,000                     200,000
Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa nini wanawake kiasi cha pesa kipo chini? Anne

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...