Na Woinde Shizza,Arusha
Serikali imetakiwa kuwaondoa wachimbaji haramu wa dhahabu katika mto yudhaya uliyopo wilayani mburu ambapo uchimbaji huo umesababisha kutokea kwa madhara makubwa katika eneo hilo likiwemo la wanafunzi wa shule kutoroka mashuleni na kukimbilia huko kufanya biashara za ngono.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo hilo,Mustapha Akunai wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na madhara yanayotokana na uchimbaji dhahabu unaoendelea katika mto huo bila mpangilio maalumu na kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Alisema mnamo mwa mwezi wa tatu dhahabu iligundulika katika mto huo na kusambaa katika maeneo mbali mbali mpaka kufikia wilaya ya Karatu hali iliyopelekea wavamiaji kutoka sehemu mbali mbali za nchi ambao wameweka makazi pembeni ya mto huo na hawana vyoo kwani maji hayo yanategemewa na wananchi pamoja na mifugo.
Aidha alifafanua kuwa wachimbaji wapatao zaidi ya 600 wamesababisha uharibifu wa mazingira na kisha kuweka mahema ambapo viongozi wote wa kiserekali wana taarifa lakini inadaiwa hakuna jitihada zozote za utekelazaji zilizochukuliwa dhidi yao.
“mimi kama mbunge na wananchi wangu nimejaribu kufanya kila jitihada za kuwaondoa wachimbaji hao imeshindikana lakini hii inatokana na wachimbaji hao kutetewa na serikali ambao nina uhakika wanahisa zao katika machimbo hayo maana wamelifumbia macho hili swala”Alisema mbunge huyo.
Aidha alieleza kuwa kutokana na wachimbaji hao kuchimba dhahabu bila mpangilio wowote yametokea madhara kama vile magonjwa ya mlipuko,wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kutoroka na kukimbilia huko huku wakifanya biashara haramu za ngono hivyo kuipelekea wilaya hiyo kurudi nyuma kimaendeleo.
Vile vile alidai kuwa endapo jeshi la wananchi linatumika kuzuia sukari inayosafirishwa nchi za jirani serilaki inawezaje kushindwa kuwazuia wavamizi hao kwani pamoja na hayo yote halmashauri hainufaiki na chochote kutoka katika dhahabu hiyo hivyo ameiomba serikali kuhakikisha inafuatilia hili swala haraka iwezekanavyo kabla wananchi hawajaamua kufatilia wao wenyewe.
Alihitimisha kwa kueleza kuwa endapo hatua hiyo ya kuwaondoa wavamizi hao watahakikisha kuwa wanamuweka muwekezaji wa kueleweka katika mto huo ambaye atakuwa akifanya hiyo biashara kwani tangu mto huo wa dhahabu kugundulika hawajawahi kunufaika na chochote kutoka katika mto huo ambapo mapato yote yatakayopatikana yataingia katika halimashauri.


Hiyo wilaya inayoitwa Mburu ni wilaya mpya? nichofahamu Mustapha Akonaay ni Mbunge wa MBULU.
ReplyDelete