Wana Chama Cha Mapinduzi Tawi la United Kingdom tunatuma salaam za pongezi za dhati kwa Dr. Peter Kafumu Dalaly kwa kuzitetea Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 na hatimaye kushinda nafasi ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga uliofanyika tarehe 02 Oktoba, 2011.

Aidha tunawapongeza wana Igunga wote kwa kufanya Uamuzi na Uchaguzi wa Busara kwa kuichagua CCM na Dr. Dalaly. Tunawashukuru viongozi na wana CCM waliojituma kuhakikisha Ushindi unapatikana. Wana Igunga wamethibitisha kuwa Uongozi na Uwakilishi Bora unatoka ndani ya CCM. 

Tunaungana nao kukukumbusha, Dr. Dalaly, kuwa tofauti ya KURA za ushindi ni ndogo na wananchi ambao hawakupiga Kura ni wengi, hivyo basi hii ni changamoto kwetu kwamba ni lazima CCM tuendelee kujisahihisha kwa kuwasikiliza wananchi na kutatua KERO zao kwa kasi ya ziada kwa kuwa wengi bado wana imani na Chama Cha Mapinduzi.

Ni wajibu wetu kukumbushana kuwa zoezi hili la demokrasia ya uchaguzi mdogo jimboni Igunga limeigharimu Taifa letu maskini fedha taslimu na rasilimali nyingi na wakati muhimu. Kwa kuwa wana Igunga wameidhamini CCM pamoja nawe ridhaa ya uwakilishi, basi ni vema:-

1. Uwalipe wana Igunga haki yao kwa kuandaa ratiba mahsusi ya kuwatembelea katika vitongoji vyao na kuandaa mkakati madhubuti utakao chochea ubunifu wa kujiajiri ili kuzalisha na kuvuna raslimali mpya za Taifa ili kuleta maendeleo jimboni.

2. Uwe mwakilishi mahiri na mshauri makini ndani ya Bunge ili Serikali na wadau wote wa maendeleo ya kitaifa wanufaike na mchango wako mpya wa mawazo.

3. Uwe chachu mpya itakayowezesha Serikali na Asasi binafsi kuweza kushirikiana kwa pamoja ili kuwafuata wananchi na kuwatengenezea mazingira yenye kuamsha vichocheo vya miradi ya maendeleo mkoani Tabora.

CCM UK tunakutakia kheri njema katika majukumu yaliyo mbele yako tukiamini kwamba utaushirikisha utashi wako, maadili ya uongozi na fikra tendaji katika kukishauri Chama, Serikali na Umma kupitia Vikao vyote halali ili kuongeza kasi ya maendeleo.

TUMEAHIDI, LAZIMA TUTEKELEZE.
Imetolewa na: CHAMA CHA MAPINDUZI -(UK)
LONDON, UNITED KINGDOM.
03 Octoba, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hawa CCM UK hawana lolote wameona wamesahaulika na wanajua kuna teuzi za ukuu wa wilaya wa TEGETA wanajua watafikiriwa hapa wana BEEP. tumewashtukia.
    tunaomba watupe jibu la mradi feki wa Opener waliotuingiza mjini.

    ReplyDelete
  2. Sasa Kafumu ukafanye kazi ya kuangalia maendeleo ya wananchi sio kwenda kulala kwenye jengo wanaigunga wanaihitaji maendeleo

    ReplyDelete
  3. Wezenu huku walihema sana tu na mijasho iliwatoka mpaka serikali yote ilihamia Igunga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...