Mwanachama wa chama cha mapinduzi wilayani Songea aliyefahamika kwa jina moja la Salome (kushoto) akimvalisha bangili zilizotengezwa kwa shanga,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma,Mhandisi Stella Manyanya katika viwanja vya mashujaa wa vita ya majimaji mjini songea.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Mhandisi Stella Manyanya,akiongea na wanawake wa wilaya ya Songea (hawapo pichani) katika mkutano wake na wanawake hao uliofanyaka jana mjini Songea.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi,Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akicheza ngoma sambamba na wasanii wa kikundi cha better cha lizabon Manispaa ya Songea mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanawake wa wilaya ya Songea katika viwanja vya makumbusho ya taifa ya majimaji mjini hapo jana.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Rukwa mhandisi Stella manyanya katikati akitoa maelekezo kwa uongozi wa makumbusho ya taifa ya majimaji mjini songea jana kuhusu umuhimu wa kuhifadhi vizuri dhana mbalimbali za kale zilizotumika wakati wa vita ya majimaji
Mwenyekiti wa bodi ya makumbusho ya mashujaa wa vita ya majimaji ya mjini songea,ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Rukwa mhandisi Stella Manyanya,kulia akisalimiana na wazee wa mila na mambo ya kale alipotembelea makumbusho hayo jana mjini songea.PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII,RUVUMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...