Baadhi ya bendera zinazotambulisha nchi wanachama zitazoshiriki mkutano wa wakuu wa nchi za madola  (CHOGM 2011 ) kuanzia Oktoba 28-30, 2011 nchini Perth -Australia ambapo Rais Jakaya Kikwete anahudhuria
  Jamani watanzania wenzangu tubadilike tuzidi kuheshimu  na kuzingatia sheria za usalama barabarani kama wenzetu wa Australia, Pichani wananchi kushirikiana na watumiaji wa vyombo vya moto wanashirikiana kufuata sheria na alama za barabarani ili kupunguza ajali zinazopoteza maisha ya wananchi,  si unaona magari hayavuki mpaka watu wapite na  watu halkadhailka wanasubiri magari yapite. tuachane na tabia ya kutoheshimu utumiaji wa alama za usalama barabarani.Picha na Mwanakombo Jumaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mjii wa kawaida sana utafikiria dar es salama

    ReplyDelete
  2. huko vigari vichache, havina haraka, kazi kulala barabarani tu, acha hizo!!!

    ReplyDelete
  3. je huyo mama hapo juu,naye anaelekeza sehemu ya kupaki na kukusanya kodi kama hapa bongo au anasafisha barabara kama wanavyofanya hapa bongo?

    ReplyDelete
  4. wametushinda usafi,sisi tunachafua tunasubiria serikali itusafishie

    ReplyDelete
  5. Angalia mji wa wenzetu ulivyo msafi, sisi Dar sijui tunashindwa vipi kuuweka mji safi!! Mambo yetu ya hovyohovyo.

    ReplyDelete
  6. Mbona hamna watu mitaani? Machinga pia hamna mwee!

    ReplyDelete
  7. Du! nimependa sana mji huu yaani umenivutia ile mbaya I wish ningelikuwa naishi hapo picha ya tano,Wanaoishi hapo wamebarikiwa.

    ReplyDelete
  8. mchangiaji hapo juu acha kutudanganya mji wa Dar es Salaam utoke wapi msafi kama huo, yani sijapata ona mji mchafu kama dar tunashindwa na manispaa za Moshi na Arusha, Halafu badala tuone changamoto mji msafi wa Australia tunasema unafanana na Dar, tuache kudanganyana, kufananisha hapo na dar ni sawa na kufananisha Kifo na usingizi. Wahusika Dar tuamke tupambane na uchafu maana ni aibu sana jiji kama Dar kuwa chafu kama lilivyo.

    ReplyDelete
  9. Wow! Michuzi umenikumbusha mbali sana! Perth is a lost heaven...Ni pazuri sana! It's a gentleman city, kila mtu ni mstaraabu. Kwa usafi ndio usiseme!

    ReplyDelete
  10. Mbona sioni cha hajabu kwenye mji huo? Mleta picha mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi nini?

    ReplyDelete
  11. Wewe uchafu asili yetu kuachana nao ni kazi kubwa kweli tembelea majengo yanayofanafan kama hayo yaliyopo Dar yanapofunguliwa na miaka miwili baadae, utaona kwanini uchafu kwetu kuondoka si rahisi

    ReplyDelete
  12. Wenzenu wana magari ya kufanya usafi tena yanawekwa sabuni na disinfectant kuondoa magonjwa ya kuambukiza na wafanyakazi wanalipwa vizuri kwa lisaa, tena wana litter kila kona namaanisha bins za kutupa taka tena zinazosomeka hivi re-cycle bin,or non-recycle. Serikali yetu hata hawajawahi kufikiri kuwa takataka zingine mali na zinasaidia kupunguza gharama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...