Baadhi ya bendera zinazotambulisha nchi wanachama zitazoshiriki mkutano wa wakuu wa nchi za madola (CHOGM 2011 ) kuanzia Oktoba 28-30, 2011 nchini Perth -Australia ambapo Rais Jakaya Kikwete anahudhuria
Jamani watanzania wenzangu tubadilike tuzidi kuheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani kama wenzetu wa Australia, Pichani wananchi kushirikiana na watumiaji wa vyombo vya moto wanashirikiana kufuata sheria na alama za barabarani ili kupunguza ajali zinazopoteza maisha ya wananchi, si unaona magari hayavuki mpaka watu wapite na watu halkadhailka wanasubiri magari yapite. tuachane na tabia ya kutoheshimu utumiaji wa alama za usalama barabarani.Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mjii wa kawaida sana utafikiria dar es salama
ReplyDeletehuko vigari vichache, havina haraka, kazi kulala barabarani tu, acha hizo!!!
ReplyDeleteje huyo mama hapo juu,naye anaelekeza sehemu ya kupaki na kukusanya kodi kama hapa bongo au anasafisha barabara kama wanavyofanya hapa bongo?
ReplyDeletewametushinda usafi,sisi tunachafua tunasubiria serikali itusafishie
ReplyDeleteAngalia mji wa wenzetu ulivyo msafi, sisi Dar sijui tunashindwa vipi kuuweka mji safi!! Mambo yetu ya hovyohovyo.
ReplyDeleteMbona hamna watu mitaani? Machinga pia hamna mwee!
ReplyDeleteDu! nimependa sana mji huu yaani umenivutia ile mbaya I wish ningelikuwa naishi hapo picha ya tano,Wanaoishi hapo wamebarikiwa.
ReplyDeletemchangiaji hapo juu acha kutudanganya mji wa Dar es Salaam utoke wapi msafi kama huo, yani sijapata ona mji mchafu kama dar tunashindwa na manispaa za Moshi na Arusha, Halafu badala tuone changamoto mji msafi wa Australia tunasema unafanana na Dar, tuache kudanganyana, kufananisha hapo na dar ni sawa na kufananisha Kifo na usingizi. Wahusika Dar tuamke tupambane na uchafu maana ni aibu sana jiji kama Dar kuwa chafu kama lilivyo.
ReplyDeleteWow! Michuzi umenikumbusha mbali sana! Perth is a lost heaven...Ni pazuri sana! It's a gentleman city, kila mtu ni mstaraabu. Kwa usafi ndio usiseme!
ReplyDeleteMbona sioni cha hajabu kwenye mji huo? Mleta picha mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi nini?
ReplyDeleteWewe uchafu asili yetu kuachana nao ni kazi kubwa kweli tembelea majengo yanayofanafan kama hayo yaliyopo Dar yanapofunguliwa na miaka miwili baadae, utaona kwanini uchafu kwetu kuondoka si rahisi
ReplyDeleteWenzenu wana magari ya kufanya usafi tena yanawekwa sabuni na disinfectant kuondoa magonjwa ya kuambukiza na wafanyakazi wanalipwa vizuri kwa lisaa, tena wana litter kila kona namaanisha bins za kutupa taka tena zinazosomeka hivi re-cycle bin,or non-recycle. Serikali yetu hata hawajawahi kufikiri kuwa takataka zingine mali na zinasaidia kupunguza gharama
ReplyDelete