Wake wa viongozi wakuu wa mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano uliofunguliwa na Malkia Elizabeth II wa Uingereza. Watano kutoka kushoto na mke wa rais Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) pamoja na baadhi ya wake wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola wakiangalia picha zinazoonyesha historia ya wenyeji wa nchi ya Australia walipotembelea makumbusho Aborigional and Torres Strair Islanders ya Perth Australia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa makumbusho ya Perth Australia wakati alipotembelea pamoja na wake wa viongozi wengine hawapo pichani waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola-(CHOGM 2011) leo.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

Na Anna Nkinda – Perth, Australia

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni mmoja wa wake wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuia ya madola waliohudhuria mkutano wa siku tatu wa jumuia hiyo unaofanyika mjini Perth nchini Australia.

Wake hao wa viongozi walishiriki ufunguzi wa mkutano huo uliofunguliwa na Malkia Elizabeth wa pili na baada ya ufunguzi waliweza kuendelea na ratiba yao ya kujifunza na kujadili mambo mbalimbali yanayaikabili jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na afya, elimu, utamaduni, mila na michezo.

Baada ya kumalizika kwa ufunguzi huo walianza ratiba yao kwa kusikiliza mada kuhusu afya ya binadamu ilitolewa na Kanali Dk. Robert Walters ambaye ni Balozi wa Serikali wa afya ya binadamu na Julian Krieg Afisa mtendaji na mwalimu wa jamii katika mpango wa mkoa wa Afya ya binadamu.

Mme wa Waziri Mkuu wa Australia Tim Mathieson aliweza kuwatembeza wake hao wa viongozi maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makumbusho ya Australia’s Aboriginal and Torres Strait Islander ambako waliweza kujifunza historia ya nchi hiyo pamoja na utunzaji wa mila na utamaduni wao.

“Asili ya wenyeji wa nchi hii ni watu weusi ambao kwa sasa kizazi chao kinatishia kumalizika kutokana na uchache wao lakini miaka ya nyuma Waingereza walihamia hapa na kuzaliana na hivyo idadi yao kuwa kubwa kuliko wenyeji hivi sasa asilimia kubwa ya waustralia ni watu weupe.

Nchi hii inaongozwa na waziri mkuu Julia Gillard’s huku mtalawala wa nchi akiwa ni Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili”, alisema Mathieson.

Katika makumbusho hayo pia walijifunza mila za watu wa Magharibi ya Australia ambao wanaishi kandokando ya Bahari ya Hindi hivyo walifahamu utawala wao, faida wanazozipata hususani za kibiashara na utalii kutokana na matumizi ya bahari na bandari ambayo ni lango kuu la meli.

Waliweza kutembelea bahari ya Hindi na kujionea shughuli za biashara na utalii zinavyofanyika katika ukanda wa pwani, meli kubwa za mizigo zinavyotia nanga, kupakua na kupakia mizigo na kuona jinsi maaandalizi ya mashindano ya kimataifa ya mchezo wa mashua (Sailing World Championships) yanayotarajia kufanyika katika mji huo mwishoni mwa mwaka huu yanavyoendelea.

Wake hao wa viongozi walishukuru kwa ziara na mafunzo waliyoyapata na kusema kuwa yatawasaidia katika kazi zao wanazozifanya kila siku ikiwa ni pamoja na kuboresha afya ya mama na mtoto na elimu ya mtoto wa kike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. chondechonde kuna mwanaume kwenye hiyo ya kwanza na ni spouse/mwenza wa mke waziri mkuu/rais sasa si vizuri kuchukulia kiuwingi na kuita wote wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...