Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakiwa wameketi wakisubiri kupatiwa mkopo wa fedha taslimu unaotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Meneja wa Vodacom Tanzania wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa akimpatia Mwanaidi Musa mkopo wa fedha taslimu kwa ajili ya kufanyia biashara zake na kuzirudisha fedha hizo bila riba yoyote,aliyekaa kushoto ni Mratibu wa Mfuko huo Ally Mbuyu.
Meneja wa Vodacom Tanzania wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa akiongea na wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,kabla ya kuanza kuwapatia mikopo ya fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini na kurudisha fedha hizo bila riba.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakimsikiliza Meneja wa Vodacom Tanzania wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa hayupo pichani ,wakati wakisubiri kupatiwa mikopo yao ya fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...