Tunasikitika kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kwamba mpendwa wetu Benedict Mpimbwe (pichani)  amefariki dunia jana saa 3:45 asubuhi ghafla jijini Dar es salaam.

Mipango ya mazishi inaendelea vyema nyumbani kwao Mbezi Luis na  misa ya mazishi itafanyika leo saa 7 mchana katika kanisa la muhimbili na baada ya hapo mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kwa mawasiliano tumia namba 0652 125858.

Naomba tushirikiane na familia katika msiba
huu mzito kwetu na familia kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Dennis LondoOctober 26, 2011

    Nimeshtushwa sana na taarifa za kifo chako,Nasikitika hatukuwahi kuonana tangu tulipoachana Kigurunyembe Sekondari mwaka 1994. Wengi tutakukumbuka kwa ucheshi na upendo wako. RIP Ben.

    Dennis Londo

    ReplyDelete
  2. BEN R.I.P DAIMA UTAKUMBUKWA KWA WEMA WAKO SITAACHA KUKUOMBEA KATIKA SALA ZANGU SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU NAAMINI SIKU MOJA TUTAKUTAKA PARADISO PARAPANDA ITAKAPOLIA
    BWANA ALITOA NA SASA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
    CLARA-ARUSHA

    ReplyDelete
  3. RIP BEN, NIMEUMIA SANA SIKUPATA MUDA WA KUKUONA AU HATA KUKUAGA. ULIKUWA MWEMA NA MCHESHI MWENYE UPENDO SANA KWA RAFIKI NA NDUGU ZAKO, "GONE TOO SOON..." TUNAJIFUNZA TU KUWA WEMA NA KUPENDANA...
    JOEL CHACHA-DAR ES SALAAM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...