mratibu wa matamasha hayo Edwin Bashir akicheza na msanii bingwa wa kuzungusha nyonga Tausi Mdegella
Umati wa wananchi wakishuhudia burudani katika mji wa mafinga
Ni umati mkubwa kweli kweli ulipata kupagawishwa kwa burudani hiyo ya Mtikisiko 2011Burudani katika uwanja wa RMA Mafinga
Na Francis Godwin, Iringa

Baada ya tamasha la Mtikisiko 2011 linaloendeshwa na kituo cha radio Ebony Fm ijumaa ya tarehe 28 mwaka huu tamasha hilo la Mtikisiko 2011 linataraji kutikisa katika mji wa Makambako wilaya Njombe kwenye viwanja vya Amani.

Mwenyekiti wa matamasha hayo ya Mtikisiko 2011 Bony Zacharia aliueleza mtandao huu kuwa katika kuhakikisha kuwa wakazi wa mji wa makambako wanatapa nafasi ya kushiriki tamasha hilo kubwa bado watapata kusindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali.

Alisema kuwa katika mji wa Makambako wasanii 20% na Belle 9 pamoja na Awilo wa Mbeya ndio watakao pagawisha katika tamasha hilo .

Wakati siku ya Jumapili tarehe 30 burudani hiyo itahamia katika mji wa Chimala wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya ambako msanii 20% MR.Blue na Awilo wa Mbeya watawasha moto katika mji wa Chimala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...