
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB (SSC) imetatizwa na hatua ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumteua mwamuzi Oden Mbaga kuchezesha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga Jumamosi ya Oktoba 29 mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa Oden Mbaga ndiye mwamuzi aliyechezesha pambano la mwisho la watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.
Pambano hilo nusura lisababishe vurugu baada ya Mbaga kukataa bao la wazi la Simba lililofungwa na Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 73 ya mchezo huo uliochezwa Machi mwaka jana.
Alibadili maamuzi yake na kukubali baada ya ama kulalamikiwa na washabiki na wachezaji wa Simba au kwa kujionea mwenyewe picha za marudio zilizoonyeshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini zilizothibitisha kuwa goli hilo lilikuwa halali.
Udhaifu huo wa kimaamuzi ungeweza kusababisha maafa makubwa uwanjani.
Ndiyo maana, Simba imetatizwa na uamuzi wa TFF kumteua tena Mbaga kuchezesha mechi hiyo, pamoja na makosa yake ya wazi aliyoyafanya katika mechi hiyo kubwa.
Simba Sports Club haina imani tena na Oden Mbaga kutokana na historia yake katika mapambano yaliyopita dhidi ya timu yetu.
Kwa taarifa hii, Simba SC inapenda kuutangazia umma kuwa japo haina imani na Mbaga, haitasusia pambano hilo kwa namna yoyote ile lakini inapenda kuweka wazi msimamo wake huo kuhusu mwamuzi huyu.
Ni matumaini yetu kuwa ujumbe huu utamfikia Oden Mbaga mwenyewe na wote waliohusika katika kumpanga awe mwamuzi katika pambano hilo.
Tunatanguliza shukrani.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba SC
Mfa maji haachi kutapatapa. Mmeshaona yule kiboko yenu amekuja sasa mnaanza kuleta malalamishi. Msianze kutafuta sababu uli mkifungwa muanze kudai kwamba mlishafahamu. Sote tunajua kuwa mbele ya Papic, Simba huwa anageukaga swala tu. Poleni sana
ReplyDeleteHuu ni mwaka wa SSC. Hata kama refa ni mwanachama halali na wa maisha wa Yanga, Jumamosi msiba ni jangwani tu come rain - come shine.. Simba inatisha - TAIFA KUBWA OOOOOOOYEEEEEEEEE...
ReplyDeleteMichezo ya kisaikolojia hiyo..YANGA WATASHIKISHWA ADABU.tafuteni fungu la kugawa tena ila ni kichapo tu. 2-0 msimbazi oyeeeee!
ReplyDeleteHII NI DANGANYA TOTO KAMA SIO UTOTO. KILA MECHI INAPOKARIBIA HUWA WANAJIFANYA KULETA COMPLAIN KAMA HIZI WAKATI WAMESHAFANYA MIPANGO YAO. HUWA HAWACHEZI MECHI BILA MIPANGO NA HIYO NDIYO KAZI KUBWA YA FRIENDS OF SIMBA LENGO NI KUWAPUMBAZA WAPINZANI WAO. INASHANGAZA KWA MTU KAMA E. KIMWAGA KUKUBALI KUANDIKA HABARI HII ILE HALI ANAFAHAMU KUWA ANAENDESHA KIPINDI CHA SPOTI KIZAA ZAA AMBACHO WENGI TUNAAMINI KINA LENGO lA KUCHOCHEA MAENDELEO YA MICHEZO KATIKA NCHI HII HUSUSAN SOKA. KWA STAHILI BASI TUTAENDELEA KUYWANGA MAJI KWENYE KINU. SIDHANI kAMA TP MAZEMBE IMEPATA MAFANIKIO KWA MTINDO HUU AU KUJAZA WABUNGE KWENYE KAMATI ZAKE, TUNATAKIWA TUBADILIKE NI AJABU KWA MTU WA KISASA KUWA NA MAWAZO YA KIZAMANI. JUZI MAN U KAPIGWA SITA KWAKE AMBAKO WATU WALIKUWA WANADAI KWAMBA HAIWEZEKANI, HATA PENATI HUWEZI KUPATA OLD TRAFORD LAKINI TUMESHUHUDIA MTU MCHEZAJI WA MAN U AKIPEWA KADI NYEKUNDU, MPIRA WA MIGUU NI MCHEZO WA WAZI JAMANI.
ReplyDeleteNi kweli kama supersport wasingekuwepo siku ile, Yanga wangeondoka na ushindi. Vile vile picha za marudio za supersport zilionesha kwamba penalty waliyopewa yanga na kupata bao haikuwa halali kwa kuwa mchezaji Mwape aliangushwa nje ya 18, sasa mechi inayokuja supersport hawatakuwepo itakuwaje? Simba inabidi ijihadhali na TFF maana inafahamika kwamba viongozi wote wa juu wa TFF ni wapenzi wa Yanga.
ReplyDeleteKAMA viongozi wote wa juu wa TFF ni Yanga mbona Yanga haiongozi ligi na imeshafungwa mechi zaidi ya moja wapenzi wa simba badilikeni. Mbona Coast Union walisawazisha goli mkwakwani likakataliwa?
ReplyDelete