Mtuhumiwa Bwana Mohamed Mwawipa (kushoto) ambaye anatuhumiwa kumshinikiza mkewe Nuru Masuba kunywa sumu baada ya kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu shilingi laki nne na elfu hamsini akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe
 Mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.


Mwili wa marehemu Nuru Masuba aliyeshinikizwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kumwibia fedha shilingi laki nne na elfu hamsini na Mumewe Mohamed Mwawipa akipelekwa kuhifadhiwa kaburini, baada ya uchunguzi wa daktari na polisi kukamilika.

Picha na habari na Mbeya yetu Blog

Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.


Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asingekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Am less speech. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen.

    ReplyDelete
  2. sasa huyo polisi hana kinga yoyote anachungulia hiyo sumu si anahatarisha maisha? mungu amlaze mahala pema peponi Nuru. amina na huyo mtuhumiwa anafaa kunyongwa hadharani

    ReplyDelete
  3. Hivi jamani huu ni ukatili wa namna gani pesa na uhai wa mtu. na je baada ya kufa pesa kazipata?

    ReplyDelete
  4. Mmmmh Kaka,

    Sasa huyo Polisi wa upelelezi ananusaje hiyo SUMU jamani, sasa kama inaleta DIZNESS si na ye analewa hapo na huyo mtuhumiwa anakimbia zake?

    Khaah! Kweli AKILI NI NYWELE

    ReplyDelete
  5. What are they waiting for he should also be killed stupid him otherwise kama ana watoto lazima watlipiza tu. Sidhani kama watampenda daima kwa kua mama yao.

    ReplyDelete
  6. Umaskini ni mbaya sana hasa ukihusisha umaskini wa fikra kama huyu jamaa!!!

    ReplyDelete
  7. Hiyo inaitwa 'contamination of evidance'. Polisi alipaswa kuvaa gloves na hakupaswa kugusa hapo hadi waje watu wa maabara, waliyosemea hayo mambo kwa ajili ya vipimo. Hilo ndilo lililofanya Knox kuachiliwa kule Italia, moja ya sababu ni kuwa polisi hawakubadilisha gloves wakati wanachukua evidence mbali mbali.
    Kuangalia kote CSI na drama za nje bado tunashindwa kununua hata gloves jamani? Au kwa kuwa ni kijijini? Eti polisi ananusa.. du

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...