KATIKA hali isiyotazamiwa na wengi, bendi mbili za Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic Modern Taarab zinatarajiwa kuvaana katika jukwaa moja Jumapili hii 30/10/2011 katika ukumbi wa Travertine Hotel – Magomeni.
Mashauzi Classic inayoongozwa na Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi imekuwa ikichukuliwa kama ndio mpinzani mkuu wa bendi ya Jahazi tangu iundwe rasmi miezi michache iliyopita.
Isha ambaye kabla ya kuunda bendi ya Mashauzi aliitumikia Jahazi iliyo chini ya Mfalme Mzee Yusuf na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia nyimbo za “Hayanifiki” na “Ya wenzenu Midomoni”.
Kwa jinsi Isha alivyoondoka bendi ya Jahazi bila kuaga imekuwa ikiaminika miongoni mwa watu wengi kuwa yeye  na Mzee Yussuf ni kama paka na panya na hivyo kupelekea onyesho hilo kuteka hisia za wapenzi lukuki wa taarab.
Isha Ramadhan amedhamiria kulitumia onyesho hilo kama sehemu rasmi ya kumuaga Mzee Yussuf na kumshukuru kwa kumjenga hadi kumfikisha hapo alipo.
Katika kunogesha zaidi onyesho hilo liliopewa jina la “Usiku wa Baba na Mwana”, Tanzania One Theatre chini ya Kapeteni Komba (Mh) imetoa jukwaa kubwa kabisa  litakalowawezesha watu kushuhudia onyesho hilo bila adha yoyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...